Header Ads Widget

DIWANI KATA YA MANDEWA-VIONGOZI WA DINI OMBEENI TAIFA AMANI NA UTULIVU IENDELEE KUTAMALAKI


*Achangisha Mil.9.4 ujenzi madarasa ya Kanisa la TAG Ginnery 

Na Thobias Mwanakatwe, SINGIDA 

VIONGOZI wa dini wametakiwa kuliombea taifa ili amani na utulivu viendelee kutamalaki katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu kwani kipindi kama hiki kunakuwa na mambo yenye viashiria vya kutaka kuvunjika kwa amani nchini.

Diwani wa kata ya Mandewa katika Manispaa ya Singida, Baraka Alli, alisema hayo jana wakati hafla ya wa harambee ya kuchangia ujenzi wa madarasa ya awali iliyoandaliwa na Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) Ginnery Calvary Temple (GCT) ambapo alifanikisha kuchangisha źaidi ya Sh.milioni 9.4.

Alisema kipindi cha uchaguzi mkuu kila mtu anakuja na staili yake ilimradi tu apate ushindi na kutawala ambapo wengine wanatumia njia mbaya za kutaka kuvuruga amani na utulivu ambavyo viliasisiwa na waasisi wetu  Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Amani Karume.

"Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na kama ambavyo ilivyo kwa miaka mingine chaguzi zinapofika kunatakiwa utuliwa wa hali ya juu  kwasababu wakati wa uchaguzi kunakuwa na mambo mengi yanajitokeza,kikubwa tunachoomba kwa viongozi wa dini mliombee taifa letu, muwaombee viongozi wa serikali na tumuombee Rais Samia Suluhu Hassan," alisema Alli.


Alli alisema wananchi lazima watambue kuwa bila amani hawawezi kukaa kanisani kuabu au kufanya chagizo lolote maana bila amani huwezi kupanga kuwa unakwenda kanisani unaweza kukuta kanisa limepigwa bomu halipo tena.

Kila mtu atakuja kwa sura nzuri lengo apate nafasi ya kuongoza lakini sio kila anayeomba kuongoza ana uwezo wa kuongoza, baba askofu tuna nafasi kubwa ya kuelimisha wananchi kwa hatujawahi kupata changamoto ya kiusalama amani na utulivu vimekuwepo muda wote na wasimamizi wetu ni CCM ambao ndio wanaongoza vizuri na ndio maana amani inaendelea kutawala," alisema Alli.

Naye Askofu wa TAG Jimbo la Singida Kati Mch.Gasper Mdimi alisema ukifanya kazi ya Mungu inakuelekeza hatima yako ilipo na kamwe huwezi kufanya kazi ya shetani halafu useme utakaribishwa na Mungu.

"Haijalishi wewe ni nani upo wapi kazi hizi zipo mbele yako wewe ndio ufanye uchaguzi Bwana Yesu mwenyewe anasema imetupasa kuzifanya kazi zake Mungu wakati tuna muda, fanya kazi ya Mungu wakati una muda utakuja wakati ambao Huna nafasi ya kufanya hivyo," alisema.

"Tukiwa na muda tufanye kazi ya Mungu kuna wakati muda hautakuwepo, wewe unakaa duniani halafu unafanya mambo kizembezembe timiza kusudu la wewe kuwepo duniani kuletwa duniani uje ule mboga mboga hayo tunayala ili tuendelee kufanya kazi ya yule aliyetuleta," alisema.

Alisema kila kazi unayotaka kuifanya unapaswa kujiuliza hiyo ni kazi ya nani na kama ni ya shetani achana nayo kama ni ya watu ipime kama inakubalika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naye Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG Ginnery Calvary Temple, Samweli Dosla, aliwashukru wananchi waliojitokeza kuchangia fedha na vifaa katika harambee hiyo na kwamba Mungu atawabariki.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI