Header Ads Widget

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA WAZIRI BITEKO KUFUATIA KIFO CHA MKURUGENZI WA TANESCO


 

Katika ukrasa wake wa X Rais Dkt Samia ameandika pia 


Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya Mhandisi Boniface Gissima Nyamohanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), pamoja na dereva wake, Muhajiri Mohammed Haule, vilivyotokea usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya barabarani eneo la Bunda, Mkoa wa Mara.

Ninatoa pole kwa familia, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko, watumishi wa TANESCO, ndugu jamaa na marafiki. 

Namuomba Mwenyezi Mungu azijaalie familia, ndugu, jamaa na marafiki subra, uvumilivu na moyo wa ibada katika kipindi hiki kigumu. 

Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. 

Amina.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI