Header Ads Widget

JUHUDI ZA MGODI WA NORTH MARA KUJENGA MAHUSIANO NA WANANCHI WAPONGEZWA

 

Na Shomari Binda-Matukio Daima

MBUNGE wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara ameupongeza mgodi wa Barrick North Mara kwa kutoa maeneo ya leseni yao kwaajili ya vijana kuchimba madini.


Pongezi hizo zimekuja baada ya siku chache zilizopita meneja wa mgodi huo Apolonary Lyambiko kuzungumza na Waandishi wa Habari na kutoa taarifa hiyo.


Akizungumza leo aprili 13,2025 kwa njia ya simu na Matukio Daima Waitara amesema hatua hiyo itaendelea kujenga mahusiano mazuri baina ya mgodi na wananchi hasa vijana kwenye mgodi huo.


Amesema hatua hiyo ya mgodi inapaswa kupongezwa na kuwataka vijana kuzingatia maeneo yatakayotolewa kwaajili ya uchimbaji na kuacha kuvamia maeneo ya mgodi kwaajili ya kutafuta dhahabu.


" Nimeona taarifa hii iliyochukuliwa na mgodi wa Barrick North Mara kwa kutoa maeneo ya leseni yao kwaajili ya vijana kujishughulisha na uchimbaji.


" Hatua hii ni jambo jema na nauomba mgodi ukamilishe mchakato huu na jambo hili litaendelea kujenga mahusiano mazuri baina ya mgodi na wananchi",amesema.


Aidha mbunge huyo amesema mgodi wa Barrick North Mara umeendelea kutoa fedha za CSR kutokana na uzalishaji wanaoufanya na zimesaidia kutekeleza miradi mbalimbali kwenye jamii.


Juzi aprili 11,2025 meneja wa mgodi huo na viongozi wa ofisi ya mahusiano ya mgodi walifanya mkutano na Waandishi wa Habari na kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo taarifa hiyo ya utoaji wa leseni.

Katika mazungumzo hayo Meneja Mkuu wa mgodi huo Apolonary Lyambiko amesema mgodi utatoa leseni zake 4 kwaajili ya kuwapa vijana kufanya shughuli za uchimbaji na jambo hilo linaendelea kukamilishwa kwa kushirikiana na serikali.


Meneja huyo amesema tayari Waziri wa Madini ameunda kamati ambayo inashughulikia jambo hilo ili liweze kuanza Mara moja.


Lengo la kutoa leseni hizo ni pamoja na kudhibiti vitendo vya uvamizi ndani ya mgodi na kuendelea kujenga mahusiano mazuri baina ya mgodi na wananchi.


Kwenye mkutano huo baina  ya mgodi na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara Jacob Mugini ameushukuru mgodi huo kwa kuendelea kufanya jitihada za kujenga mahusiano na kuwashirikisha Waandishi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI