Header Ads Widget

RAIS DKT SAMIA AMEFANYA MAKUBWA TUZIDI KUMUOMBEA -AIDAN MLAWA


Aidan Mlawa mdau wa maendeleo Kilolo 


Na Matukio Daima Media 

Wakati waumini wa dini ya Kikristo wakiadhimisha Jumapili ya Matawi siku muhimu inayokumbusha kuingia kwa Yesu Kristo Yerusalemu kama Mfalme wa Amani – ni muda pia wa kutafakari juu ya thamani ya amani katika maisha yetu ya kila siku kama Taifa. 


Ifahamike kuwa Amani siyo jambo la kawaida au la kupuuzwa, bali ni zawadi kubwa ambayo kila Mtanzania anapaswa kuitunza na kuilinda kwa nguvu zote.



Mdau wa maendeleo wilayani Kilolo mkoani Iringa Aidan Damian Mlawa anasema kuwa Kila mmoja ana wajibu wa Kulinda amani yetu.

Kuwa Tanzania imejijengea sifa kubwa kimataifa kama kisiwa cha amani barani Afrika. Hii ni matokeo ya mshikamano wetu kama Watanzania, utamaduni wa maelewano, heshima kwa taasisi za kiserikali na juhudi za viongozi wetu waliotangulia na waliopo katika kuhakikisha misingi ya amani inaimarika. 

"Hasa katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, taifa limeendelea kushuhudia hatua mbalimbali za maendeleo zinazotokana na mazingira tulivu na salama".

Kuwa Dkt. Samia amejipambanua kama kiongozi mwenye dira na busara na amekuwa akiendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu, huduma za kijamii kama afya na elimu, pamoja na kuimarisha mahusiano ya kimataifa.

Kwani  Juhudi hizi zote haziwezi kufanikiwa bila kuwepo kwa amani ya kweli. Hivyo basi, ni jukumu letu kama wananchi kuenzi kazi hii kwa kuilinda amani iliyopo.

"Katika wakati huu ambapo tunakaribia uchaguzi mkuu, kuna umuhimu mkubwa wa kuimarisha mshikamano na kupuuza kauli, vitendo au propaganda zozote zinazoashiria kuvuruga amani."

Alisema kuwa  Uchaguzi ni mchakato wa kidemokrasia unaopaswa kufanyika kwa utulivu, heshima na kuheshimu maoni ya wengine. 

Vyama vya siasa, wanasiasa, viongozi wa dini, wazazi, vijana, na makundi yote ya kijamii vina wajibu wa kusimama kidete kuhimiza amani na kudhibiti lugha au matendo yenye viashiria vya uchochezi

"Waumini wa dini zote – iwe ni Wakristo, Waislamu, Wahindu, Wabudha au wengineo – wanayo nafasi ya kipekee ya kuhakikisha ujumbe wa amani unafika kila kona ya nchi yetu"

Alisema kuwa  Viongozi wa dini wamekuwa mstari wa mbele katika kuhubiri maadili mema, upendo na uvumilivu – misingi ambayo inaimarisha amani ya kweli. 

"Lakini hata wasio na dini, wao pia ni sehemu ya jamii yenye dhamana ya kuishi kwa mshikamano na kushirikiana katika kujenga Taifa lenye utulivu"Alisema Mlawa

Kuwa Tanzania ni nchi yetu sote hakuna atakayetuletea amani kutoka nje kama hatutaamua kuilinda sisi wenyewe. Ni wajibu wa kila mmoja wetu, kuanzia kijijini hadi mijini, kuhakikisha tunatenda yaliyo ya haki, tunaheshimu sheria na taratibu, tunakemea kwa nguvu zote wale wanaotaka kuvuruga umoja wetu. 

"Tuwabeze na kuwapuuza wote wasiolitakia mema Taifa letu Amani yetu ni maisha yetu, Tusipoilinda, basi tunahatarisha kila hatua ya maendeleo tuliyopiga na kuififisha ndoto ya kizazi kijacho"

Mlawa alisema kuwa Tujivunie utulivu wetu, tuendelee kuishukuru serikali yetu kwa kuendeleza mazingira salama ya kuishi, kufanya biashara, kuabudu, na kupata huduma muhimu. 

"Tuendelee kumuombea Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili aendelee kuongozwa na hekima na afya njema katika kutimiza majukumu yake ya kuliletea taifa letu maendeleo ya kweli kwa wa pamoja, tuseme: Amani yetu ni Maisha Yetu"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI