Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Watu 11 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya biashara ya watoto kwa kuwapeleka kufanyakazi ya kuchunga mifugo katika kata ya Ninga Wilayani Njombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga mbele ya Vyombo vya habari anasema watu hao waliwapeleka watoto 14 katika kijiji cha Lima na kuwafanyisha kazi ya kuchunga Ng'ombe kinyume cha sheria.
Amesema watoto hao walitolewa mkoani Songwe na hivyo watuhumiwa pamoja na watoto wote wamerejeshwa Songwe kwa hatua zaidi za Kisheria.
Aidha Kamanda Banga amesema pia wamewakamata watu wawili wanaojihusisha na wizi wa Simu kwa kutumia Pikipiki huko katika kijiji cha Nundu.
Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya madereva Bodaboda mjini Njombe ambao wanasema wengine sio bodaboda bali wanatumia pikipiki kuiba.
Pia wanaonya tabia ya watu kuwatumikisha watoto badala ya kuwaacha wasome.
0 Comments