Tume huru ya Uchaguzi nchini inaendelea na mafunzo kwa watendaji ngazi ya Jimbo kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Mafunzo hayo yanafanyika leo hii katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze. Mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku mbili mfululizo tarehe 06-07/02/2025.
Kauli mbiu ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ni “Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa Uchaguzi Bora.”
0 Comments