Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Dr.Venance Mwasse amefanya mazungumzo na Kamishina wa Magereza Zanzibar ndugu Khamis Khamis ili kufanikiza azima yao yakuachana na matumizi ya kuni na kutumia nishati safi ya kupikia ya Rafiki Briquettes.
Mkurugenzi huyo wa STAMICO amefanya mkutano huo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa nishati safi na salama ya kupikia huko Zanzibar.
Dkt . Mwasse amefanya mkutano pia na Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Dr. Islam Salum pamoja na mambo mengine wamejadili namna wanavyoweza kuisaidia jamii visiwani Zanzibar kufikiwa na nishati kupikia ya Rafiki Briquettes kwa kuzingatia sasa nchi inategemea kupiga marufuku uzalishaji wa kuni na mkaa na utekelezaji wa Sera ya nishati safi na salama.
Kwa upande wake Kamishina wa Magereza ameishukuru STAMICO na Mkurugenzi Mtendaji kufika ofisini kwake na kuonesha nia kuisaidia magereza kuhamia katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia ya Rafiki Briquettes na kuahidi kutekeleza yote yaliyoelezwa ili Magereza ya Unguja na Pemba kunufaikana nishati ya RafikiBriquettes. Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt.Venance Mwasse alikuwa Zanzibar kufuatia mualiko wa Katibu Mkuu.
0 Comments