Watu 14 wamefariki na wengine wanane kujeruhiwa katika ajali iyohusisha lori la mizigo lililokuwa linatokea Dar es saalam kwenda Morogogoro na Coaster iliyokuwa inatokea Morogoro kwenda Dar es salaam usiku huu December 18,2024 eneo la Mikese barabara kuu ya Morogoro - Dar es salaam.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Morogoro Nkungu Daniel amethibitisha kupokea kwa miili hiyo na majeruhi ambapo amesema waliofariki bado miili yao haijatambulika.
Nkungu amesema kati ya marehemu 14 Wanaume wanane na Wanawake ni 6 huku majeruhi wakiwa wanaendelea na matibabu katika Hospitali hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima, amefika Hospital ya Rufaa Mkoa Morogoro wanakopatiwa matibabu majeruhi hao ambapo ametoa wito Wananchi kufikia katika Hospitali hiyo Ili kutambua miili ya Ndugu zao.
Katika ajali hiyo Madereva wotew amefariki Matukio Daima media inaendelea kufanya jitihada za kulipata Jeshi la Polisi kwa taarifa zaidi.
KARIBU JAZA MAFUTA MAGERE OIL IGINGILANYI ISIMAMI BARABARA KUU YA IRINGA -DODOMA 0741239118
0 Comments