Header Ads Widget

TAKUKURU,YAOKOA EKARI NANE ZA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA BUGANGO KAGERA

.Na Shemsa Mussa -Matukio daima App.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imeendelea kutekeleza majukumu mbalimbali katika kipindi Cha julai Hadi Septemba 2024 ikiwemo uokoaji wa hekari 8 za Ardhi katika Kijiji Cha Bugango kata Kakunyu Wilaya Missenyi Mkoani Kagera.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoani humo katika ukumbi wa ofisi hizo Ndg Ezekia Sinkara,Naibu Mkuu wa Takukuru Kagera amesema kwa kipindi Cha julai Hadi Septemba mwaka huu wameweza kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kuwasaidia wananchi wa Kijiji hicho kupata eneo lao la Ekari 8 zilizokuwa zinamilikiwa na Mtu mwingine kinyume na makubaliano.

" Kupitia Mkutano wa hadhara tulioufanya kwenye Kijiji hicho Tarehe 12/07/2024 kwa lengo la kupokea kero mbalimbali za wananchi zinazohusiana na rushwa,mkazi mmoja alisimama na kutoa taarifa ya kuwepo mtu anayemiliki eneo lenye ukubwa zaidi ya eneo alilopewa na Kijiji kwa mujibu wa taratibu,amesema Sinkara "

Aidha Sinkara,amesema kuwa katika kipindi hicho  Takukuru imeweza kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo  jumla 18 yenye thamani ya Bilioni 144,993,472,267.16) na kubaini miradi 10 kati ya hizo yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.137 kuwa na mapungufu yaliyohitaji marekebisho ikiwa ni sawa na asilimia 55.55 % ya miradi iliyofuatiliwa.

Katika uchambuzi wa Mifumo 2 Mfumo wa utendaji kazi wa mabaraza ya Ardhi ya kata pamoja na Mfumo wa utendaji kazi wa vyama vya akiba na mikopo Saccos,na kusema kuwa katika programu ya Takukuru rafiki  katika kipindi hicho wamezeza kuzifikia kata 12 na kupokea kero mbalimbali kutoka katika sekta ya Afya,Elimu,Maji,Kilimo,Ujenzi Fedha na Nishati na kero hizo zimefikishwa kwa watoa huduma kwa ajili ya utekelezaji na ufuatiliaji unaendeleaje.

Pia Sinkara amesema kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa unaotalajiwa kufanyia  November 27 ,wamejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wananchi pamoja na makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa kisiasa,watia nia kuhakikisha zoezi Hilo linafanyika bila kuwepo vitendo na viashiria vya rushwa.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI