Header Ads Widget

TAKUKURU WAOMBWA KUONGEZA MAPAMBANO YA RUSHWA KWENYE TAASISI ZA SERIKALI



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wananchi mkoani Njombe wameitaka Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Njombe kuongeza nguvu ya mapambano ya Rushwa kwenye Taasisi za Serikali zinazotajwa mara kwa mara kujihusisha na vitendo vya Rushwa pamoja na utoaji huduma duni.


Kauli za Wananchi hao zinakuja kufuatia ripoti ya Takukuru ya Utendaji kazi katika kipindi cha miezi mitatu ambapo Naibu mkuu wa Taasisi hiyo mkoa wa Njombe Noel Mseo anasema kumeripotiwa malalamiko ya wananchi wakilalama juu ya vitendo vya Rushwa na utoaji huduma duni huku kada ya Afya ikitajwa kuongoza kwa malalamiko,Ardhi,Polisi na Mahakama.


Katika Ripoti hiyo Naibu mkuu wa Takukuru pia amesema kupitia ukaguzi walioufanya kwenye miradi mbalimbali wamebaini mapungufu madogomadogo kwenye miradi mitano yenye thamani ya shilingi milioni 579 ambayo wametoa maagizo kurekebishwa haraka.


Baadhi ya wakazi wa Njombe akiwemo Tenende Mwakagile Amesema serikali kwa serikali wamekuwa na tabia ya kubebana pindi wanapotenda maovu hivyo Takukuru wafanyekazi yao kwa weledi.


Wengine akiwemo James Mhenga wamesema kada ya Afya inapaswa kujirekebisha katika utoaji wake huduma kwani hairidhishi.


Masuala ya uchaguzi ni miongoni mwa ajenda ambazo Takukuru wamesisitiza hasa kujiepusha na Rushwa katika Kuwapata viongozi kwani kuna madhara makubwa ya kuwachagua viongozi kwa njia ya Rushwa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI