Header Ads Widget

KAMBAYA AMG'OA KIGOGO CHAMA CHA ACT WAZALENDO LINDI

  

Chama cha ACT wazalendo kimepata pigo tena baada ya kingunge wa chama hicho ambae alikuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya siasa na mipango ya uchaguzi Hamisi Msagula kukihama chama hicho na kutimkia chama cha mapinduzi

Tukio hilo limefanyiaka Jana huko Katika kijiji cha mtumbikile halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani Humo ambapo Kada wa chama cha mapinduzi bwana Abdala kambaya alimpokea rasm na kumkaribisha Katika chama Chao


Mkutano huo ulioudhiriwa na viongozi wa chama na wananchi wa kijiji cha mtumbikile na Maeneo jirani ulikuwa na dhamira ya kunadi Sera za chama cha mapinduzi sambamba na wagombea wa chama hicho wa Serikali za mitaa vijiji na vitongoji

Akizungumza mara baada ya kujiunga na chama hicho Msagula alisema ni faraja kubwa kwake kuona ameungana na wanachama wapenda Maendeleo ambao mara zote wamekuwa na Sera zinazotekelezeka





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI