Header Ads Widget

CHONGOLO ATOA MIEZI NANE SORECU KUONGEZA IDADI YA VYAMA WANACHAMA KUFIKIA ASILIMIA 95.

                                    MKUU WA MKOA WA SONGWE, DANIEL CHONGOLO


Na Moses Ng'wat, Mbozi.


MKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, ameupongeza uongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Songwe (Sorecu) kwa kufanikisha ukarabati wa jengo la ofisi,  huku akielekeza uongozi huo na Mrajis Msaidizi wa Mkoa kuhakikisha hadi kufikia Mwezi Juni,2025 wanaongeza idadi ya vyama  wanachama na kufikia asilimia 95.


Chongolo ametoa maelekezo hayo, Novemba 15, 2024 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa chama hicho, ambapo kabla ya mkutano huo alianza na shughuli ya  alizinduzi wa  jengo la ofisi za chama zilizopo Mjini Vwawa, Wilayani Mbozi.




Amesema uongozi wa Sorecu umefanya kazi kubwa ya kuleta umoja na utulivu kwa wanachama,  ikiwemo kufanya jitihada za kufanikisha  ukarabati wa jengo la ofisi.


"Niwapongeze kwa umoja wenu na kuamua kuenzi jitihada zilizofanywa na watangulizi wenu ambao waliona mbali na kuamua kujenga majengo kwa ajili ya Ushirika ambayo leo nimezindua rasmi baada ya ukarabati kukamilika,  ombi langu kwenu ni kuhakikisha kuwa ofisi zilizokarabatiwa zinatumika kwa manufaa ya wanachama na wakulima ili wanufaike na ushirika wao"


Hata hivyo, Chongolo alisema idadi ya vyama wanachama hairidhishi kulinganisha na idadi halisi ya vyama vya ushirika vya Msingi vilivyopo, hivyo kuutaka uongozi wa Chama  Kikuu na Mrajis Msaidizi kuhakikisha hadi kufikia Mwezi Juni,2025 Vyama wanachama wa SORECU wanafikia angalau asilimia 95.



Pia, alisisitiza Menejiment ya Chama Kikuu na Ofisi ya Mrajis Msaidizi inaandaa Program maalum ya mafunzo kwa wajumbe wote wa bodi watakao chaguliwaili kuwaandaa kufanya kazi kwa uadilifu na weledi. 

 

Vile vile amewaagizamaofisa Ushirika katika Halmashauri zote wahakikishe wanasimamia Vyama vya Msingi na kuendelea kuwekeza zaidi kwenye elimu ya Ushirika na Masoko ili wakulima wazidi kunufaika na uwepo wa Ushirika katika maeneno yao.


Aidha, Chongolo, alisisitiza elimu ya Mfumo wa Stakabadhi gharani iendelee kutolewa zaidi kwa wakulima na viongozi wote ili kuhakikisha kila mtu anakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu  mfumo unavyofanya kazi na manufaa yake.


Kuhusu suala la tozo ya Ushuru wa mazao, ametoa rai kwa Halmashauri na Vyama vya Ushirika kuhakikisha  sheri inafuatwa kikamilifu ili kupunguza malalamiko kwa walipa ushuru ikiwa ni pamoja na kukaa vikao vya kutoa elimu kwa walipaji hawa.  


Awali akitoa taarifa , Meneja wa Sorecu, Mon Mwampamba, alisema ukarabati wa jengo hilo la ofisi umegharimu kiasi cha shilingi 73.6 Milioni .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI