SHIRIKA hilo la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) limetoa msaada huo ambao umefadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Watu wa Korea unalenga kuunga juhudi za serikali ya Tanzania katika kupunguza vifo vya watoto wachanga na kuongeza matumaini ya akina mama kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi 76.3 milioni, vimepokelewa mapema leo Oktoba 16, 2024 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika ofisini kwake na baadae kukabidhi vifaa hivyo kwa waganga wakuu wa Halmshauri za Mkoa huo.
0 Comments