Header Ads Widget

MAAFISA WANNE WA OYA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI KIBAHA

 


Wafanyakazi wanne wa Taasisi ya Mikopo almaarufu kwa jina la OYA leo tarehe 16 Oktoba ,2024 wamefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia na kumuua Juma Said Seif (45), mkaazi wa Kitongoji cha Mbagala Mlandizi Mkoani Pwani mnamo Oktoba 7 mwaka huu.

Akisoma shitaka hilo Wakili wa Serikali Monica Mwela mbele ya Hakimu Mkazi Muandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha Emmaeli Lukumai, amesema kuwa kesi hiyo yenye namba 29566 2024 ambayo imesomwa kwa mara ya kwanza.

Aidha Wakili wa Serikali Mwela amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Dastan John Charles (23) mkazi wa Kilangalanga Mlandizi, Abdallah Felix Wendiliwe (32) mkazi wa Janga Mlandizi, Christopher John Charles (23) mkazi wa Kilangalanga na Emmanuel Joshua Olala(24) mkazi wa Kilangalanga Mlandizi Kibaha Vijijini. 

Baada ya kusikiliza shitaka hilo la mauaji, Mheshimiwa Hakimu Mkazi Muandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Lukumai amesema kuwa kesi hiyo ya tuhuma za mauaji ya kukusudia ambayo imefikishwa kwa mara ya kwanza ushahidi bado haujakamilika hivyo kesi hiyo itasomwa tena Oktoba 30 2024 ambapo watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.

Aidha watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI