Na Fatma Ally Matukio DaimaApp,Dar
Naibu Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amesema ifikapo mwaka 2030 watu million 300 katika Bara la Afrika wawe wamefikiwa na umeme ili watu wengi waweze kutumia nishati safi ya kupikia.
Ameyasema hayo mapema leo hii alipokua katika uzinduzi wa mkutano wa 9 wa siku 2 wa soko la Nishati Afrika ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hotel ya Hayyat.
Amesema kuwa, Benki ya maendeleo ya Afrika imepima kutoka kwa wadau wake wanapata fedha kutoka kwao imeonekana Tanzania imepiga hatua kubwa sana na wamefanikiwa, hali iliyopelekeanchi hiyo kuwa shamba darasa kwa wenzao kwenye usimamizi wa Sekta ya nishati.
Aidha, amesema jambo jengine ni kwamba mkutano huo utakua ni maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi wa Afrika wanaokwenda kujadili masuala ya nishati kwenye bara la Afrika kwani kuwapata watu 300 sio kazi rahisi kuishia kwenye ngazi ya Wizara.
Ameongeza kuwa, lengo la mkutano huo ni kwenda kujadili na kufanya tafakuri kubwa kama bara juu ya upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia ambapo mfumo wake unachangamoto nyingi kwenye utekelezaji wake.
"Watu wengi wanalalamika gharama ni kubwa, sasa ni lazima kueka mikakati mizuri ili kuhakikisha gharama za upatikanaji wake uwe rahisi na watu waweze kumudu"amesema Waziri Dkt Biteko
Aidha, amesema nchi Tanzania imepata heshima ambayo haikua kazi rahisi bali kutokana na mausiano mazuri ya kidiplimasia kati ya nchi hiyo na Benki ya maendeleo ya Afrika ambapo wamekiri Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye masuala ya kisera na usimamizi, uzalishaji na usafirishaji na upelekaji wa umeme Vijijini.
Kwa upande wake, Makamo Mwenyekiti wa Nishati, mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji wa kijani AFDB Dr Kevin kairuki wameamua kufanya kazi kwa pamoja na Tanzania kwa sababu ipo mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
"Tanzania imekua ikitilia manani mambo ya nishati safi ndio sababu tukakaa na wadau kama vile World Benki tukasema hili kongamano lifanyike Tanzania kwani kupata watu million 300 wa kutumia nishati safi ya kupikia sio rahisi" amesema Dr Kairuki.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Eng Felchesmi Mrama amesema mkutano huo wataweza kujadiliana ukuaji wa Nishati, matarajio, namna ya kuipata, uzalishaji na ujumuishaji wa Sekta binafsi kwani ifikapo 2034 wanataka nishati ipatikane kwa unafuu.
0 Comments