WAKATI Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kiendelea kutoa Msimamo wake juu ya maandamano ,mdau wa maendeleo Kilolo mkoani Iringa Aidan Mlawa amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake wa hekima katika kuzuia maandamano yaliyopangwa kufanyika yenye viashiria vya uvunjifu wa amani .
Mlawa alisema kuwa hatua hiyo ililenga kudumisha amani na utulivu nchini. Kwa mujibu wa Mlawa, amani ni msingi wa maendeleo ya taifa lolote, na hatua ya Rais Samia ni ya busara, hasa katika kipindi hiki ambapo Tanzania inahitaji utulivu ili kuendeleza mipango ya maendeleo.
Akizungumza na Matukio Daima media leo Mlawa alisisitiza kuwa maandamano ya kisiasa mara nyingi hupelekea vurugu na migawanyiko, jambo ambalo linaweza kusababisha kudorora kwa uchumi na usalama wa nchi.
"Tunaona mataifa mengine duniani jinsi maandamano yanavyoathiri uchumi, biashara, na maisha ya wananchi. Hatutaki kuona hali hiyo nchini kwetu," alisema
Mlawa, akiongeza kuwa hatua ya Rais Samia ni ishara ya kujali ustawi wa wananchi na kulinda maendeleo ambayo tayari yameanza kupatikana chini ya utawala wake.
Aidha, Mlawa aliwakemea wanasiasa wanaopandikiza chuki za kisiasa na kuchochea migawanyiko nchini.
Alisema kuwa siasa za chuki hazijengi bali zinaharibu mshikamano na maendeleo ya jamii.
"Tunahitaji siasa za kujenga taifa, siasa ambazo zinalenga kuleta maendeleo na umoja, si kuchochea uhasama miongoni mwa wananchi," alisema.
Pia Mlawa alitoa wito kwa wanasiasa kutumia majukwaa yao kuhamasisha mshikamano na amani, badala ya kutumia siasa kama chombo cha kugawanya watu.
Alisema iwapo Taifa litakuwa na amani na utulivu, basi maendeleo ya kiuchumi na kijamii yataendelea kwa kasi, jambo ambalo litawanufaisha wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa.
Mlawa aliwasihi Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuimarisha uchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi.
"Amani ni msingi wa maendeleo, na kwamba kila mwananchi ana jukumu la kuhakikisha kuwa Tanzania inasonga mbele kwa utulivu tambua ni muhimu tuelewe kuwa hatuwezi kupata maendeleo bila amani tuunapaswa kuwa kitu kimoja kama taifa," Mlawa.
Mapema Jana mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe kupitia mitandao ya kijamii alisisitiza Kuwepo kwa maandamano hayo .
Huku jeshi la Polisi Nchini likiweka mkazo wake kuwa piga marufuku maandamano hayo .
Kuwa maandamano hayo yana viashiria vyote vya uvunjifu wa amani Nchini.K
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro ametoa Kauli hiyo leo Jumapili Septemba 22.2024) kuwa Jeshi hilo lilipokea taarifa ya chama hicho kuhusu dhamira ya kufanya maandamano hayo, taarifa ambayo ilijibiwa kwa kuelezwa kuwa maandamano husika yamepigwa marufuku hivyo yeyote atakayefanya kinyume na hapo atashughulikiwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria.
0 Comments