Header Ads Widget

TAKUKURU NJOMBE YAWANOA WANAHABARI JUU YA UCHAGUZI

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati mamlaka ya serikali za mitaa  na Tawala za Mikoa TAMISEMI ikitangaza Novemba 27 mwaka huu kuwa ni Tarehe ya  Uchaguzi wa Serikali za mitaa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imekutana na wanahabari kuwaeleza viashiria vya rushwa na Namna ya kuisaidia jamii kupambana navyo.



Kamanda wa Takukuru mkoa wa Njombe Ephrem Cassim wakati wa mafunzo kwa wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari anasema nafasi ya vyombo vya habari ni kubwa katika jamii na hivyo wananchi wanapaswa kupata taarifa sahihi na kwa Wakati namna ya kukabiliana na vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi.


Aidha Kamanda Cassim ameonya dhidi ya wanasiasa wanaojipitisha na kugawa zawadi katika kipindi hiki kwa lengo la kutaka kuchaguliwa katika uchauguzi na kwamba hawatoachwa salama.


Mwanasheria wa Takukuru mkoa wa Njombe Ng'anzo Saidi anasema sheria zitachukuliwa kwa wanaokiuka kanuni za uchaguzi kwani jamii inatakiwa kuwapata viongozi waadilifu wasio na shaka katika upatikanaji wao.


Naye mkuu wa Dawati la Uzuiaji Rushwa mkoa wa Njombe Akoheki Mbapila anasema licha ya ushahidi kuwa kikwazo katika mahakama ili kuwatia hatiani wahusika lakini ni lazima mapambano yaendelee.


Kwa upande wao wanahabari mkoani Njombe akiwemo Dickson Kanyika,Prosper Mfugale,Steven Ngole na Emmanuel Kalemba wanasema elimu waliyoipata itakuwa msaada mkubwa kuelekea katika uchaguzi huo na kwamba imewapa urahisi wa kufanya kazi yao.


Vitendo vya rushwa vinapaswa kupingwa kwa vitendo na kila Mtanzania mzalendo ili kusaidia taifa kupiga hatua kimaendeleo kwani vinakwamisha jitihada za serikali za kuwasaidia wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI