Header Ads Widget

MWENYEKITI WA ACT NCHI HAIWEZI KUENDELEA KAMA KIONGOZI HANA MAONO

Na MWANDISHI WETU, PEMBA 

MWENYEKITI Taifa wa Chama Act Wazalando Othman Masoud Othman amesema nchi yoyote duniani haiwezi kupata maendeleo bila ya kiongozi kuwa na maono, kusimamia msingi ya utawala bora na kuthamini Wananchi wake kwa sababu wao ndio Wafalme waliweka Serikali madarakani.

Othman Masoud Othman ameyasema hayo wakati akihutubia maelfu ya Wananchama wa chama hicho katika mkutano wa hadhra uliofanyika katika uwanja wa Mpira wa konde Polisi, Jimbo la Konge Wilaya ya Mcheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alisema duniani kuna visiwa vidogo kuliko Zanzibar lakini vna uchumi imara kutokana na kuwa na mipango mizuri na maono ya viongozi yatakayo waletea maendeleo Wananchi wake na baadhi ya visiwa hivyo ndege zinatua habarini.

“Wilaya ya Micheweni ina utajiri mkubwa wa ardhi yenye ukubwa wa kilomita za Mraba 231 sawa na Mkoa wa Mjini Mgharib Unguja huku kukiwa na utajiri wa Rasilimali za baharini na ardhi lakini ndio wilaya inayoongoza kwa umasikini na utapia mlo kwa Watoto,”

Alisema Wilaya ya Micheweni ni eneo ambalo lipo karibu na Mombasa Kenya na mwambao wa Tanga Tanzania bara lakini limeshindwa kutumika kuleta mapinduzi ya kiuchumi kutokana na kukosekana a miondombinu ya uhakika ya uchukuzi na usafirishaji.

Alisema Matatizo ya umasikini yanawavamia mpaka Walimu ambao walipata heshima kubwa katika miaka ya nyuma lakini sasa wanalazimika kufanya kazi za bodaboda kujiongezea kipato na mahitaji huku baadhi ya maofisa wa Polisi wakistaafu wanalizimika kufanya kazi makonda wa daladala kutokana na maslah duni na mafao wanayoyapata.

Nae Makamu  Mwenyekiti wa Act Wazalendo  Taifa Ismail Jussa Ladu amesema katika kipindi cha miaka 60 ya uongozi wa Serikali ya CCM wameshindwa kuifungua kisiwa cha Pemba kiuchumi kutokana kukosekana kwa bandari ya kisasa na Uwanja wa ndege wa kimataifa.

Alisema wananchi wa Pemba wanakabiliwa na tatizo kubwa la mfumuko wa bei za vyakula baada ya mchele aina ya  mapembe kilo moja kuuzwa 2400 na kuwapa wakati mgumu Wananchi wenye kipato cha chini kutokana na gharama za usafirishaji wa mizigo kuwa mara mbili kabla ya kuingia Pemba kutoka nje ya nchi kupitia bandari ya Malindi.

Alisema Serikali ya Awamu ya nane Agost 31 mwaka huu imekiri hadharani kuwa Zanzibar ina kiwango kikubwa cha umasikini wa mahitaji ya Mwananchi, ukosefu wa ajira, udumavu wa Watoto kwa asilimia 30 kutokana na lishe mbovu pamoja na ukosefu wa ukuwaji wa teknolojia.

“Maneno haya sisemi Jussa amesema makamu wa Pili wakati akizindua Dira ya mpango wa maendeleo ya Taifa 2025 katika shughuli iliyofanyika huko Tunguuu,”

Jussa ambae kitaaluma ni mwanasheria alisema wakati wa kampeni za mwaka 2020 chama Tawala kilitoa ahadi za kuzalisha ajira laki Tatu lakini mpaka sasa vijana wamehitimu vyuo vikuu hawana ajira Zaidi ya kuwaachia madeni wazazi wao kuwasomesha kwa kukopa,”

Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wa chcma hicho Omar Ali Shehe alisema vitendo vya kibaguzi vimeanza kujitokeza kuelekea uchaguzi kama ilivyojitokeza miaka ya nyuma baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Chama cha Act Wazalendo kinaendelea na mikutano ya hadhra huku wakitumia muda mwingi kukosoa Serikali ya Awamu ya Nane kuwa imeshindwa kuondoa tatizo la ajira na kusimamia misingi ya uwajibikaji na kupiga vita vitendo vya rushwa na ufisadi hasa katika miradi ya maendeleo.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI