Header Ads Widget

MWANAMKE ATOLEWA UVIMBE WA KILO 7 TUMBONI

 


NA MATUKIO DAIMA App, BUKOBA

Jopo la Madaktari wa upasuaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba(BRRH) limefanikiwa kufanya upasuaji na kutoa uvimbe mkubwa kwenye ovari wenye kilogram 7 kutoka kwa mwanamke mwenye umri wa miaka 31.

Upasuaji huo mkubwa umefanyika Septemba 23,2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba.


Akieleza baada ya kumalizika kwa upasuaji huo,Bingwa wa Upasuaji wa jumla wa Hospitali hiyo, Dr. Laetus Mwombeki alisema kwamba upasuaji huo umemalizika vizuri na mgonjwa anaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa mama wa mgonjwa huyo (jina lake limeifadhiwa)amewashukuru madaktari kwa kufanikisha upasuaji huo huku akieleza kuwa mtoto wake amesumbuliwa na uvimbe huo kwa takribani miezi minne.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI