Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania Mdude Nyagali Mpaluka amemtaka katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwawajibisha viongozi wa Serikali kwa kushindwa kulinda raia na mali zao.
Mdude ameeleza hayo wakati akitoa maoni yake baada ya katibu mkuu wa CCM kudai kuwa Chama Cha Mapinduzi hakihusiani na masuala ya masuala ya utekaji.
Katibu mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameonyesha bayana kwamba Chama Cha Mapinduzi CCM, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla hawahusiki na utekaji unaodaiwa kuwepo nchini ambapo kiongozi huyo mtendaji mkuu wa CCM ameielekeza Serikali kuharakisha uchunguzi huo.
Mdude Nyagali Mpaluka mwanaharakati na mwanachama wa CHADEMA anasema CCM ndio yenye Serikali hivyo kutowawajibisha viongozi wa Serikali ni kulea uovu ambao unajulikana na watu anaosema wakubwa.
Mwanaharakati huyo na muambata wa sauti ya wa-Tanzania anasema kutokana na kusuasua kwa uchunguzi wa matukio ya utekaji na mauaji nchini ndio maana jamii inapata mashaka na kuhusika kwa mamlaka za Serikali hivyo kutaka wachunguzi wa nje ya nchi kwenda Tanzania kuchunguza matukio hayo.
Hivi karibuni jeshi la Polisi kupitia mkuu wake IGP Camilius Wambura alinukuliwa akisema hali ya amani nchini Tanzania iko shwari.
0 Comments