Header Ads Widget

WANANCHI KAJEJEJ KUNUFAIKA NA MIRADI YA NYUKI

Viongozi wa Shirika lisilo la kiserikali la Kugoma Development Organization wakiwa katika kikao cha kujadili mradi wa ufugaji nyuki na uhifadhi wa mazingira unaotekelezwa katika kijiji cha Kajeje wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WANANCHI wa Kijiji cha Kajeje wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wanatarajia kunufaika na mradi wa ufugaji nyuki unaotekelezwa na Shirika la Kigoma Development Organisation (KDO) kupitia mradi wa uhifadhiwa na utunzaji mazingira wa msitu wa Masito.

Mratibu wa mradi huo,Hussein Ruhava unoajulikana kama Ufugaji wa nyuki kwa uboreshaji wa uhifadhi na usimamizi wa msitu wa Masito alisema kuwa kupitia ufugaji wa nyuki mradi unalenga kukuza shughuli za kiuchumi kwa wanakijiji na kuongeza usalama wa kipato huku wakilinda msitu na mazingira ya msitu huo.

Katika utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa kwa ruzuku kutoka Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) kiasi cha shilingi milioni 12 kinatarajia kutumika kwa mradi huo wa mwaka mmoja ambapo wananchi 27 wa Kijiji hicho cha Kajeje wilaya ya Uvinza wakitarajia kunufaika na mradi moja kwa moja.

“Mradi utatoa mafunzo kwa washiriki 27, Wanachama wa KDO pamoja na wananchi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi ya msitu wa masito/Mkanka juu ya mbinu bora za ufugaji nyuki, urinaji wa asali, uchakataji wa asali, usindikaji asali, ufungashaji wa asali, uhifadhi wa asali na mbinu za utafutaji wa masoko sambamba usimamizi na uhifadhi wa mazingira hifadhi ya misitu,”alisema Hussein Ruhava Mratibu wa mradi huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa KDO, Neema Paul alisema kuwa tayari shirika hilo limeshapokeaa malipo ya awali ya shilingi milioni tano ambazo zitahusika na utoaji wa mafunzo kwa walengwa na ununuzi wa mizinga ya awali 38 kati ya mizinga 80 inayotarajia kununuliwa na kugawiwa kwa walengwa.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika awamu ya pili ya mradi huo wa mwaka mmoja watapokea pia kiasi cha shilingi milioni tano ambapo watanunua mizinga 42 na kwamba mradi huo utaongeza kipato cha wananchi hao sambamba na kuhifadhi na kutunza mazingira yam situ huo wa Masito.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI