Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Tellack amewataka wananchi wa Mkoa huo kuunga mkono na kushiriki kikamilifu Katika kutoa maoni ya kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 ikiwa ni sehemu ya kutengeneza Tanzania tuitakayo.
Tellack ametoa Rai hiyo Katika kikao cha ukusanyaji WA maoni ya Wadau kuhusu Dira ya Taifa 2050 kwa Ngazi ya Mkoa kilichofanyika huko manispaa ya Lindi .
Dira hii ya Taifa ya maendeo ya miaka 25 itaanza kutumika rasmi mwaka 2026 hadi 2050 na hapa Baadhi ya Wadau wa kikao hicho wanatoa maoni Yao juu ya Dira waitakayo.
Katika Karne hii ya 21 imekuwa na ushindani mkubwa wa kutawaliwa na uwezo wa kiteknolojia , uzalishaji wa tija miundombinu imara ya mawasiliano na uchukuzi na nguvukazi yenye hurka ya kujituma hivyo kama Mkoa na Taifa ni wakati sasa wa kujiimarisha Katika Maeneo hayo ili kuweza kushiriki kikamilifu badala ya kuwa wasindikizaji.
Amesema madhumuni ya Dira hiyo ni kuamsha ,kuunganisha na kueleza juhudi na fikra fikra na rasilimali za Taifa Katika Maeneo muhimu yatakayowezesha kufikia malengo ya maendeo kwa miaka 25 hijayo na ili kuweza kustahimili ushindani mkubwa wa kiuchumi uliopo duniani.
" Maandalizi ya Dira ya maendeo 2050 haina buni kuungwa mkono na wananchi wote ndio maana Katika kuiandaa Serikali inakusanya maoni kutoka kwa Wadau mbalimbali ili Dira hiyo iweze kupata ridhaa ya Wananchi wengi kutoka sehemu zote za Jamii yetu"
0 Comments