Header Ads Widget

CHADEMA MBEYA WAIHUSISHA CCM, SERIKALI KUZUIWA KONGAMANO LA BAVICHA.

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mbeya kimesema haitavumilia kile kinachoitwa hujuma za jeshi la Polisi na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kuwanyanyasa wanasiasa hasa wa upinzani.


Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Mbeya Masaga Pius Kaloli, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho mkoani Mbeya.

Masaga amesema kitendo cha Polisi kuzuia kongamano la vijana lililokuwa lifanyike Agosti 12 mwaka huu kitaifa mkoani Mbeya kimeleta taswira mbaya kwa nchi na kwamba kiliratibiwa na Serikali.


"Ndugu zangu waandishi wa habari, najua wako askari wenye nia njema kwa mfano RPC Kuzaga wa hapa Mbeya kuna muda alikuwa anataka mazungumzo na si kutumia nguvu lakini wako askari wengi wlaiotumika kihuni kutukamata na viongozi wetu wengi na wanachama kupigwa akiwemo Mhe.Sugu sasa haya mambo hatuwezi kuyavumilia, naomba makundi yote katika jamii tuungane kukemea haya wakiwemo machifu, wachungaji tunapoona maovu kama haya tujitokeze kukemea", amesema Masaga Kaloli, Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Mbeya.

Naye mwenyekiti wa Baraza la vijana wa Chama hicho (BAVICHA) mkoa wa Mbeya Evaristo Elisha Chonya, amesema Serikali ya Tanzania ilibariki kuzuiwa kwa kongamano hilo kwasababu ya hofu na mashaka ya nguvu ya upinzani zama hizi za kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.


Chonya anasema vijana mkoani Mbeya wanapendekeza kongamano lao lifanyike mwezi ujao au oktoba 2024 ili kukidhi kiu ya vijana kote nchini na wananchi kwa ujumla.

"Ninachelea kusema Serikali ya CCM imepigwa upofu, kuamini kwamba kumiliki virungu, fimbo za umeme, mabomu, magari ya kijeshi na askari wanaoamini katika matumizi ya nguvu kuliko akili ni mtaji wao kukaa madarakani bila ridhaa ya wananchi naamini ni kujilisha upepo. Matendo ya kinyama ambayo Serikali imekuwa ikitufanyia yanajenga chuki na hasira miongoni mwetu", ameeleza Chonya na kuongeza:


"Sisi sio wajinga kiasi cha kuendelea kuvumilia udharimu nyakati zote, jambo linaloweza kuwahakikishia ni kwamba saa yaja ambayo kila msharimu atatoa hesabu ya udharimu wake akidhani kufanya udharimu huo ni sifa na sisi vijana tunasema kama hawatabadilika hicho wanachokitafuta muda sio mrefu watakipata ", amesisitiza Elisha Chonya, kiongozi wa BAVICHA mkoa wa Mbeya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI