Header Ads Widget

CCM WILAYA MANYONI YATOA AĜIZO UJENZI MAABARA SEKONDARI YA KAMENYANGA IKAMILIKE HARAKA

 


NA Thobias Mwanakatwe,Manyoni  

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida kimetoa mwezi mmoja kwa serikali kusimamia umaliziaji wa ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari Kamenyanga ili wanafunzi waanze kuitumia haraka.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Manyoni, Jumanne Makhanda,ametoa agizo hilo leo (Agosti 26, 2024)  baada ya Kamati ya Siasa Wilaya hiyo kutembelea na kukagua ujenzi wa maabara katika shule hiyo ambayo ipo kata ya Aghondi ikiwa ni ziara ya kuangalia utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata hiyo.



Makhanda alisema maabara hiyo ambayo serikali ilitoa Sh Milioni 30 ni muhimu ikamilike haraka ili wanafunzi hususani wa madarasa ya mitihani waweze kuitumia kwa ajili ya kuandaa na mitihani hali itakayoongeza ufaulu wa masomo.


Alisema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi sana katika wilaya hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo ya sekta ya elimu hivyo kinachotakiwa ni kwa watendaji kuhakikisha wanaisimamia iweze kukamilika ndani ya mkataba.


"Tunampongeza sana mheshimiwa Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutujali sana sisi wilaya ya Manyoni ametupa fedha nyingi sana lakini sasa watendaji tumwangushe tuhakikishe miradi inakamilika kwa wakati," alisema Makhanda.


Awali Mkuu wa Shule ya Sekondari Kamenyanga kisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi miwili alisema shule hiyo ilipokea Sh.milioni 42.5 kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya somo la Biolojia na ukamilishaji wa chumba kimoja cha darasa.



Alisema wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo, walichangia nguvu zao kwa kuchimba msingi  na kujaza kifusi vyenye  dhamani ya Sh.200,000.


Alisema ujenzi wa maabara hiyo umechelewa kukamilika kwasababu fundi aliyepewa zabuni ya kujenga alikosea kujenga 'chamber' wakati tayari ameshalipwa fedha zake zote.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI