Header Ads Widget

MWENYEKITI WA BODI RUWASA AKOSHWA NA KASI YA UENDELEVU WA MRADI WA MAJI NYANGAO, RUANGWA NA NACHINGWEA

 


NA HADIJA OMARY, LINDI.


Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya wakala wa maji na usafi wa mazinginra vijijini (RUWASA) mhandisi lucy koya  ameonyeshwa kuridhishwa na Kasi ya ujenzi wa Mradi wa maji wa Nyangao, Ruangwa, Nachingwea unaotekelezwa na mkandarasa Emirates Builders contraction Limited kwa gharama ya zaidi ya bilioni 119.


Atua hiyo imekuja baada ya  mwenyekiti huyo kufanya Zihara Mkoani Lindi akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa RUWASA mhadisi Clement kivegalo ya kukagua na kuangalia utekelezaji wa miradi ya maji vijijini iliyohusisha kutembelea matangi kwa ajili ya Mradi huo,nyumba za watumishi na ofisi, vituo vya kusukuma maji pamoja na eneo la chanzo cha Maji.



Amesema kutokana na Kasi ya uendelevu wa Mradi huo ni Imani yake kuwa utakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika  na huduma hiyo.


Clement kivegalo ni Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Amesema  Mradi huo utakapokamilika anatarajia kuhudumia vijiji sita kutoka Wilaya za Lindi Ruangwa na Nachingwea ambapo uzalishaji wake wa maji kutoka kwenye chanzo unatarajiwa kuwa ni wa wastani wa Lita za ujanzo 15,000,000, kwa siku huku mahitaji ya vijiji hivyo ni Lita milioni 6 kwa siku.



Hata hivyo aliongeza kuwa  Utekelezaji wa Mradi huo unaenda kutimiza adhima ya Serikali ya kufikisha huduma ya maji vijijini kwa asilimia 85 ifikapo mwaka 2025.


Meneja wa Mradi huo kutoka kampuni ya Emilet contractions Said Msangi Amesema Mradi huo kwa sasa umekamilika kwa asilimia 40 na kwamba wamejipanga kuukamilisha kwa wakati.



 katibu wa Waziri Mkuu jimboni bwana Ramadhani Matola Amesema  mradi huo utakuwa na msaada kwa wananchi wa  Ruangwa kupata maji Safi na salama


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI