Header Ads Widget

MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA SIHA KUTEMBELEA MIRADI SITA YA BILIONI 6.933...

 


NA WILLIUM PAUL, SIHA. 


MWENGE wa  Uhuru hatimaye umepokelewa katika wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ambapo unatarajiwa kuzindua miradi sita yenye thamani ya Bilioni 6.933.



Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge huo ukitokea wilaya ya Hai, Mkuu wa wilaya ya Siha, Dkt. Christopher Timbuka alisema kuwa, Mwenge huo utakimbizwa kilomita 196 kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbali mbali. 



Alisema kuwa, Mwenge huo utatembelea darasa la Watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Sanya juu ili kuona namna ambavyo wanafaidika na matunda ya Serikali ya awamu ya sita. 



Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa, pia utashuhudia upandaji miti ikiwa ni kumbukumbu ya kutunza mazingira ambapo wilaya hiyo imeshapanda miti mingi katika kipindi hiki cha mvua lengo likiwa ni kutunza mazingira. 

Mwisho... 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI