Header Ads Widget

KILIO CHA JIJINI MBEYA WAIANGUKIA SERIKALI KUHUSU FIDIA UJENZI WA NJIA NNE.

 


Wananchi wa eneo la Simike ikiwemo mtaa wa Kilimahewa Kata ya Mabatini jijini Mbeya wanailalamikia Serikali kupitia Wakala wa ujenzi wa Barabara Tanzania (TANROAD) Mkoa wa Mbeya kwa kuwachelewesha kutoendeleza maeneo yao kwa madai kuwa watalipwa fidia tofauti na sasa ambapo wengi wao wameambiwa hawatalipwa fidia.

Wakizungumza na kituo hili katika eneo la Simike, wananchi hao kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Kata za Mabatini na Nzovwe, wamesema awali Serikali iliwataka kutoendeleza maeneo yao ya pembezoni mwa barabara ili kupisha mradi wa ujenzi wa barabara ya njia nne lakini kwa sasa wamepewa taarifa kuwa baadhi yao ndio watapewa fidia.

Wananchi hao wanaishangaa Serikali kwa kuleta mkanganyiko huo kwani tangu mwaka 2016 walitakiwa kutoendeleza makazi yao hadi watakapoanza kulipwa na kwamba hivi karibuni ndipo walipewa miezi sita kuwa wataanza kulipwa kuanzia Aprili 2024 lakini mwezi uliopita (Mach 2024) ndipo walipewa taarifa za kuwa sio wote watakaolipwa.

Akizungumzia suala hilo ofisini kwake, Meneja wa Wakala wa ujenzi wa Barabara Tanzania (TANROAD) Mkoa wa Mbeya Mhandisi Masige Matari, amesema fidia itatolewa kwa wale wanaofuatwa na barabara ikizingatiwa ni umbali wa mita 22.5 za eneo la hifadhi ya barabara.

Amewatoa hofu wananchi wanaopitiwa na mradi wa upanuzi wa barabara hiyo kubwa kwani Serikali ina mpango mzuri wa kimaendeleo kwa kuwalipa fidia watakaotakiwa kupisha barabara na si wote watakaolipwa kwasababu hawafikiwi na mradi huo.

TANROAD Mkoa wa Mbeya inasema mara kadhaa imekuwa ikifanya mazungumzo na wananchi hao ikiwemo maeneo ya Mbalizi na Nzovwe ili kuendelea kutoa elimu hiyo kwa wananchi ili Serikali kufikia azma yake ya kujenga barabara ya njia nne kuwa njia sita ili kuchochea maendeleo hivyo katika kutimiza azma hiyo njema ni vema Serikali ikaendelea kuketi na wananchi hawa ili kuelewana kwenye mpango huo wa utolewaji fidia ikizingatiwa wananchi hao hawajaendeleza makazi yao tangu walipositishwa mwaka 2016 huku baadhi wakilazimika kuwahamisha wapangaji wao ili kupisha mradi huo wa ujenzi wa barabara.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI