Header Ads Widget

CCM - MBINGA WAMEJIPANGA KWA MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA CCM BALOZI DKT EMMANUEL NCHIMBI





    Na Amon Mtega

          Mbinga.

BAADHI ya Wapenzi na  Wanachama  wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wamejipanga vema na mapokezi ya ziara ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi atakaye wasili Wilayani humo Aprili 22 mwaka huu . 


Akizungumza na matukio Daima kuhusu ziara hiyo katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Mbinga John Bosco Mkandawile amesema kuwa Wanachama na wapenzi mbalimbali wa chama hicho wamejipanga vema kwenye mapokezi hayo huku wakiwa na shauku ya kukutana na kiongozi huyo.


Mkandawile amesema kuwa Katibu Mkuu huyo atapokelewa eneo la Mhekela nje kidogo ya Mji wa Mbinga na kuwa akiwa kwenye ziara hiyo atazungumza na baadhi ya Viongozi wa chama pamoja na Wananchi wote kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Wilayani humo.


 Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo Mbinga mjini Jonas Mbunda hivi karibu wakati akizungumza na Wananchi alisema Wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Bolozi Dkt Emmanuel John Nchimbi .


Mbunge Mbunda pia aliwataka na Wanachama wa Vyama rafiki (UPINZANI)pamoja na Viongozi wao kushiriki mapokezi hayo kwa kuwa katibu mkuu huyo ndiye anayesimamia Ilani ya utekelezaji ya CCM ambayo inatekelezwa na Serikali.


          Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI