Header Ads Widget

REA, STAMICO ZAJIPANGA NISHATI SAFI YA KUPIKIA INAPATIKANA VIJININI


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

JUMLA ya Shilingi Bilioni 5 zimetengwa kwaajili ya Mradi wa ununuzi wa mashine kubwa tatu za uzalishaji wa makaa ya mawe lengo likiwa ni kuhamasisha matumizi  ya mkaa mbadala (Mkaa salama) kama chanzo cha Nishati safi ya kupikia. 


Mhandisi, Advera Mwijage, Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Mbadala ameyasema hayo jijini Dodoma walipotembelewa na Makamu wa Rais Dkt, Philip Mpango kwenye banda lao la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwenye Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake 


Amesema REA kwa kushirikiana na STAMICO imefadhili ununuzi wa mashine hizo kubwa tatu kwa ajili ya kuzalisha makaa ya mawe nakuwa REA inatekeleza jukumu la kuhakikisha nishati za aina zote zinapatikana vijijini na kwa Watu wote .



"REA kuwa imekuwa mstali wa mbele kuwasaidia Waendelezaji wa teknolojia za nishati safi pamoja na Miradi inayolenga kwenye kuongeza upatikanaji wa bidhaa za nishati safi ya kupikia, " Amesema mhandisi Advera 


Mhandisi, Advera ameongeza kuwa" katika mwaka huu wa fedha wa 2023/2024, Wakala imetoa zaidi ya mitungi ya gesi ya kupikia 158,100 kwa Wananchi wa vijijini kama sehemu ya hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuongeza kuwa mitungi zaidi ya laki 4 itatolewa kupitia utaratibu huo, "


Mhandisi, Advera amesema kuwa, mbali ugawaji wa mitungi ya gesi, REA imeanza kutekeleza program ya kusambaza gesi asili kwa Wananchi wa vijijini wa mkoa wa Pwani na Lindi, Mradi huo una thamani ya shilingi bilioni 6.8 ambapo kwa kuanzia kaya zaidi 980 zitaunganishwa kwenye mtandao wa gesi asilia kwenye nyumba zao.


Ameutaja Mradi mwengine ni wa kuwaunganisha Wananchi wa vijijini katika mkoa wa Pwani na Mtwara kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). 


"Mradi huu una thamani ya shilingi bilioni 13.5 ambapo kwa kuanzia kaya zaidi ya 1,400 zitanufaika, " Amesema mhandisi Advera.


Amesema REA pia inatekeleza Mradi wa ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza, ambapo Tanzania kuna magereza zaidi ya 129 ambapo imeelezwa kuwa matumizi ya kuni pekee yake ni zaidi ya asilimi 93. Mradi huo umeanza kutekelezwa na utagharimu shilingi bilioni 40.


Amesema Miradi mingine unaofanana na huo ni ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambapo kambi 26 zitanufaika na Mradi huo uliotengewa zaidi ya bilioni 3.5 ambapo utaanza kutekelezwa hivi karibu.


Mradi wa Mmwisho ambao REA imepanga kuutekeleza ni wa kujenga miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye shule kongarobaini za sekondari hapa nchi, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 2.6 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI