Header Ads Widget

OPARESHENI KALI YA USALAMA BARABARANI IRINGA ,KAMISHINA SISIWAYA AONGOZA

 


Mkuu wa oparesheni wa kikosi Cha usalama barabarani nchini Kamishina msaidizi wa polisi Nassoro Sisiwaya amefanya oparesheni Kali katika mkoa wa Iringa ya kukagua magari ya abiria na mizigo .

Mkuu huyo wa Oparesheni wa kikosi Cha usalama barabarani akiwa na kaimu mkuu wa kikosi Cha usalama barabarani mkoa wa Iringa ASP .Glory Mtui   wamefanya ukaguzi huo Leo katika barabara ya Iringa -Morogo na Iringa -Mbeya huku akitoa onyo Kali kwa madereva wazembe .


Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi eneo la kituo Cha ukaguzi wa magari Check Point ) Igumbilo mjini Iringa ,mkuu huyo wa Oparesheni amesema kuwa lengo la oparesheni hiyo ni kuendelea kubaini madereva wazembe wasio zingatia Sheria za usalama barabarani pamoja na ubora wa vyombo vya moto .

Hivyo aliwataka madereva kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa vyombo vyao kabla ya kuingia barabarani na kuwa wasio fanya hivyo watakutana na mkono wa Sheria .

Huku akiwataka wakuu wa vikosi vya usalama barabarani mikoa yote nchini kuendelea na oparesheni hizo .

Kaimu RTO mkoa wa Iringa ASP Glory Mtui amesema mkoa wa Iringa umejioanga kuendelea na oparesheni hizo na kuwataka madereva kuzingatia Sheria za usalama barabarani.
















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS