Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Ukatili mkubwa kwa wanawake nchini unatajwa kuchagizwa na uchumi duni na hivyo wanapaswa kuamka kwa kufanyakazi zitakazowaingizia kipato.
Katika muendelezo wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayotarajia kufikia tamati machi 8 mwaka huu Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Njombe Mhe.Beatrice Malekela akiwa mgeni wa heshima katika maadhimisho ya wanawake wa kata ya Luponde halmashauri ya mji wa Njombe amesema heshima katika familia itajengwa kwa uchumi Imara unaomuhitaji mwanamke kuchakarika.
Aidha Jukwaa la wanawake kata ya Luponde chini ya afisa maendeleo kata Gladness Sanga Umeona ni muhimu kusherekea sherehe hizo kwa kuwatembelea wahitaji wanne wenye changamoto mbalimbali na kuwapa mahitaji huku Diwani wa viti maaalumu tarafa ya Igominyi Catherine Mwalufuna akiwataka wananchi kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji.
Felisia Mwageni na Florida Mwageni ni baadhi ya wanawake toka kata ya Luponde ambao wanakiri kuwapo kwa mfumo dume kwenye baadhi ya familia ambao inapaswa kupingwa na kila mmoja.
Naye Ofisa maendeleo ya jamii kata ya Uwemba Irene Mlonganile Amewataka wanawake kuwa makini na watoto wao kwani ukatili umekuwa ni mkubwa unaopaswa kutazamwa kwa karibu.
Machi Nane kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya Wanawake ambapo kwa Mkoa wa Njombe maadhimisho hayo yanafanyika Ulembwe wilayani Wanging'ombe kwa Kauli mbiu isemayo''''Wekeza kwa mwanamke kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii
0 Comments