Header Ads Widget

BEYOND GIVING TANZANIA WAJA NA KAMPENI YA GONGA KENGELE ILI KUHAMASISHA WATOTO WENYE ULEMAVU KUPELEKWA SHULE.

Afisa Elimu, Elimu maalum awali na Msingi James Mgabo

Mkurugenzi wa shirika la Beyond giving Tanzania Joseph Msuka

NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.

Shirika la Beyond giving Tanzania Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza limeanzisha kampeni  ijulikanayo kama (Gonga Kengele) Kwa ajili   ya kuhamasisha jamii ili iweze kuwatoa ndani watoto wenye ulemavu na kuwaandikisha Kwa ili kuanza elimu ya awali na Msingi.


Akizungumza na wananchi katika Mkutano wa adhara wa kuhamasisha wananchi kuwatoa ndani watoto wenye ulemavu Mkurugenzi wa shirika hilo Joseph Msuka amesema kuwa Kila Mtoto anawajibu wa kupelekwa shuleni na sio kuwafungua ndani.

Msuka ameeleza kuwa kampeni waliyoianzisha itasaidia watu wengi ikiwemo jamii ya watu wa kisesa kutokana na wengi kutokuwa na uelewa juu ya umuhimu wa watoto wenye ulemavu kuwandikishwa ili waweze kuanza shule kama watoto wasiokuwa na ulemavu wanavyokwenda shule.

"Nimeamua kufanya kampeni hii Kwa ili kuhamasisha jamii inayoishi na watoto wenye ulemavu Kwa ajili kuanza kuwaandikisha waweze kuanza shule" Alisema Msuka.


James Mgabo ni Afisa Elimu, Elimu maalum awali na Msingi Wilaya hiyo Amesema kuwa wazazi wanapaswa kujitokeza kuwaandikisha watoto wenye ulemavu wanaopaswa kuanza elimu ya awali na Msingi bila kubagua kwani elimu ni haki ya Kila mtu.

Mgabo ameeleza kuwa Kila Mtoto anawajibu wa kupatiwa elimu na sio kuwa bagua watoto wenye ulemavu na kushindwa kuwapa haki yao na kuendelea kuwabagua katika jamii.


"Elimu ndio silaha na mkombozi pekee kwani tusipowapa elimu watajiona wanyonge na kuona wametengwa na jamii" Alisema Mgabo.


Clara Stanslaus ni mmoja wa wazazi mwenye Mtoto mwenye ulemavu ameeleza hakuwa na elimu yoyote juu kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu .


" Mimi Nina Mtoto mlemavu sikuwa na uelewa wowowte juu ya kupeleka shule kupitia Mkutano huu umenifungua macho kumbe na wenye ulemavu wanahaki ya kwenda shule" Amesema Clara.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI