Header Ads Widget

WAHUKUMIWA KWA MAKOSA UBAKAJI WENGINE WAKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

 




WATU watatu mkoani Pwani wamehukumiwa vifungo tofuati kutokana na kukutwa na makosa ya ubakaji na ulawiti.


Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo akielezea mafanikio ya jeshi hilo kwa kipindi cha mwezi Agosti.


Lutumo amesema kuwa watuhumiwa hao ni Salim Issa ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kulawiti mwingine ni Albino Anthony amehukumiwa kifungo cha miaka 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka.


Amesema mwingine Mazoea Salum amehukumiwa kifungo cha miaka 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka huku Hamisi Idd amehukumiwa kifungo cha miaka 20 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali.


Aidha amesema kuwa Yusuph Athuman naye  amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali.


Katika hatua nyingine jeshi hilo kwa kushirikiana na na askari wa wanyama pori wamefanikiwa kukamata watubuhumiwa 14 wakiwa na nyama ya swala na magamba 11 ya mnyama Kakakuona.


Lutumo amesema kuwa kukamatwa watuhumiwa hao 14 ni mafanikio ya jeshi hilo ambapo kati ya hao watuhumiwa watatu wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI