Na MWANDISHI WETU ZANZIBAR
KUFUATIA Kuhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi za utekelezaji wa mradi wa barabara za ndani kwa gharama nafuu umeisukuma Bodi ya Mfuko wa Barabara Tanzania kuja kujifunza namna ya utekelezaji wa miradi hiyo visiwani Zanzibar
Utekeleza wa mradi wa barabara za ndani Wizara ya ujenzi Mawasiliano na uchukuzi kwa niaba ya serikali ya mapinduzi zanzibar imetumia teknolojia ya gharama nafuu juu ya ujenzi wa barabara za ndani utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha hali ya usafiri na usafirishaji wa mazao kwa wananchi
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Khadija Khamis Rajab amesema ziara hiyo inalenga kukuza mashirikiano na uzoefu wa hatua za utekelezaji wa mradi wa barabara za ndani unaotekelezwa hapa Zanzibar kwa kilomita 275.9. ambao unagharimu Dola za Marekani Milioni Themanani ($ 80,300,000) unguja na Pemba
Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa barabara kutoka Tanzania bara Octavian Mshiu amesema hatua hiyo imekuja kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzanzia mama Samia Suluhu Hassan ya kuwataka kuja kujifunza namna Zanzibar inayotengeza barabara zao kwa gharama nafuu.
Mratibu wa barabara za ndani Zanzibar Cosmas Msolwa ameyasema hayo wakati kuwasilisha taarifa fupi ya ujenzi wa barabara za ndani kwa kiwango cha lami (Double Surface Dresingi/chip Seal) yenye urefu wa kilomita 275.9 amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika Julai 2025, ambao unasimamiwa na wakala wa barabara Zanzibar.
0 Comments