Header Ads Widget

UVCCM MOSHI VIJIJINI WAPEWA SOMO..

 Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI


JUMUIYA ya vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro wamepewa somo katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Katika mkutano wa baraza kuu la umoja huo lililofunguliwa na Said Kineng'ena ambaye ni katibu wa siasa na uhusiano wa jumuiya ya wazazi taifa amewakukumbusha vijana hao majukumu Yao.

Katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika katika ofisi za CCM wilaya ya Moshi Vijijini vijana ambao ni wajumbe halali walipata wasaa kwa kupewa darasa juu ya ya majukumu Yao kama viongozi.

'Nakushukuru mwenyekiti Yuvenail Shirima kwa kunialika ila japo Nina majukumu mengine naomba kuwapa darasa kidogo maana na mimi nimetokea kwenye hii jumuiya'anasema

Anasema miongoni mwa majukumu ya umoja wa vijana hao(UVCCM)ni pamoja na kulinda chao yaani CCM kwa njia yoyote ile.

'Nawakumbusha tuu sehemu ambazo kama umoja wa vijana mkumbuke wajibu wenu ni pamoja na kuwalinda viongozi wenu hususani katika mikutano yao'anasema

Yuvenail shirima ambaye ni mwenyekiti wa UCCM wilaya ya Moshi Vijijini amekiri kwa mara kadhaa kuelewa darasa hilo ambalo pia anadai litakuwa chachu kwenye uongozi wake.

'Niseme nimepata somo kutoka kwa aliyetutangulia alichok

isema tunaenda kukifanyia kazi Kwa maslahi ya ya jumuiya lakini n



a chama pia'anasema

Kwa mujibu wa Shirima ni kuwa jukumu lililopo mbele yao sasa ni pamoja na kuwasemea viongozi wao keep wa kile kinachofanyika ikiwa ndio dhima ya umoja huo.

'Tumekumbushwa wajibu kama vijana ni lazima tutoke na tuseme haya yanayofanyika tusirisi nyuma hata kidogo 'Anasema

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI