Header Ads Widget

UFAWAZA WAMSHUKURU MBUNGE MAVUNDE KWA UDHAMINI WA BIMA

 




Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


UMOJA wa Familia ya wanamichezo wa zamani Dodoma(UFAWAZA) wamewasilisha rasmi shukrani zao kwa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kwa udhamini wa Huduma ya Bima ya NISHIKE MKONO inayotolewa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB).


Mwenyekiti wa  UFAWAZA Ally  Kheri ametoa shukrani hizo leo jijini Dodoma mbele ya Mbunge Mavunde kwa kuwa karibu na kuusaidia umoja huo tangu kuanzishwa kwake tarehe 27 November 2021 .


Pia Mbunge Mavunde amesaidia  udhamini wa malipo ya Shilingi 3,600,000 kwa wanachama 75 kwa ajili ya  _BIMA YA NISHIKE MKONO_ ambapo mwanachama anayepata matatizo ya kufiwa hulipwa kiasi cha 1,200,000- 5,000,000.




Kwa Upande ,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa kilimo Anthony Mavunde ameshukuru (UFAWAZA) kwa kutambua mchango wake na kuahidi kuendelea kushirikiano nao katika kuinua michezo Jijini Dodoma.


“Nanawashukuru kwa kutambua mchango wangu kwenye umoja wenu huu na nitaendelea kuwa nanyi bega kwa bega na kuhakikusha hatumuachi mtu nyuma ," amesema Mbunge Mavunde.


Aidha Amesema Dodoma tumejipanga vizuri kuwapa heshima na kutambua mchango wa wanamichezo wa zamani.


"Tatizo la mmoja ni tatizo letu sote,na furaha ya mmoja ni furaha yetu sote,tutahakikishia tunausimamia huu umoja ili uwe msaada wa kweli kwa wanamichezo wa zamani," Amesema Mbunge Mavunde.


Amebainisha kuwa Pamoja  na Bima hiyo ya NISHIKE MKONO  hatua inayofuata ni ya kupata uhakika wa Bima ya Afya ambapo kwa mujibu wa taratibu lazima wafikie idadi ya wanachama 100 ndio waingie kwenye mfuko wa UMOJA AFYA wa Bima ya Taifa.


 "Tukikamilisha takwa hilo la usajili nitawachangia Shilingi 5,000,000 kwa ajili ya malipo ya mfuko wa UMOJA AFYA”Alisema Mavunde




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI