Header Ads Widget

SERIKALI YATENGA BILIONI 150 KWA AJILI YA RUZUKU YA MBOLEA

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt.Stephan Ngailo amesema mpango na bajeti wa Mamlaka mwaka wa fedha 2023/2024 Ruzuku ya Mbolea Serikali imetenga bajeti ya Shilingi 150 Billioni kwa ajili ya ruzuku ya Mbolea.


Hayo ameyasema leo jijini jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari 


Amesema Mamlaka itaendelea kuratibu na kusimamia utoaji wa ruzuku kwa wakulima, Mpango wa Maendeleo wa Kilimo wa II (ASDPII),Kuimarisha tija na faida katika kilimo kwa kuboresha upatikanaji na ufikiwaji wa pembejeo za kilimo.


Amesema Mamlaka imekuwa na itaendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya mbolea kwa njia mbalimbali, kuongeza mtandao wa wasambazaji wa mbolea nchini.


Amesema kutokana na kupanda kwa bei za mbolea katika soko la dunia, Serikali ilitenga fedha kwa ajili ya kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima kwa lengo la Kupunguza gharama ya mbolea, Kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, Kuimarisha usalama wa chakula, Kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani



“Mbolea za kupandia na kukuzia zinahusika katika mpango wa ruzuku kulingana na mahitaji, Mfumo wa kidijitali (Digital Platform) unatumika kuratibu usajili wa wanufaika, usambazaji, mauzo na malipo ya fedha za ruzuku” 


Na kuongeza "mpaka kufikia Juni 30,2023 upatikanaji wa mbolea ulikuwa tani 1,115,841 ambapo lengo limefikiwa na kuvuka kabla ya miaka miwili ya ilani kukamilishwa kwa asilimia 139.48," .


Alisema pia kuongeza upatikanaji wa mbolea kutoka tani 586,604 mwaka 2019/2020 hadi tani 800,000 Mwaka 2020/2025;


Lakini pia amesema kuwa ilani inaelekeza kuimarisha ukaguzi wa mbolea, mbegu na viatilifu kwa kuanzisha na kuimarisha ofisi za Kanda nchini ili, Mamlaka imeanzisha Kanda Tano ambazo nip0a



“Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa na Kanda Mashariki”alisema.


Hata hivyo mpango wa maendeleo wa miaka mitano awamu ya tatu ni pamoja na kuendelea kujiimarisha katika masuala ya ushindani katika viwanda kwa ajili ya maendeleo ya watu.


Amesema kufungua fursa za kiuchumi, kujenga uchumi wa Viwanda, kuimarisha ushindani wa ndani na wa kikanda na masoko ya kimataifa.


"Katika kujenga uchumi wa viwanda kilimo kinachangia asilimia 65 ya malighafi za viwandani," Amesema .


Nakuomgeza kuwa Mamlaka itaendelea kuhamasisha uwekezaji wa Viwanda vya kuzalisha mbolea nchini na kuwa kitovu cha mbolea katika ukanda huu wa Africa Mashariki na SADC," Amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI