Header Ads Widget

RAIS DKT MWINYI ATOA MWALIKO KWA TIMU ZA KIMATAIFA KWENDA ZANZIBAR


RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amezikaribisha nchini timu za kimataifa kuja kujionea haiba na mandhari nzuri ya visiwa vya Zanzibar na vivutio vya utalii vilivyomo.


Dk. Mwinyi aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na timu ya “Kaizer Chief” kutoka Afrika Kusini iliyoalikwa nchini ya timu ya Wananchi “Yaung Aficans”, Yanga.


Alisema, Zanzibar ni kisiwa cha utalii chenye vivutio vingi vya Fukwe za bahari na Hifadhi ya kimataifa ya Mji Mkongwe, hivyo aliikaribisha timu ya “Kaizer Chiefs” kuitumia fursa ya uwepo wao nchini kutembelea baadhi ya vivutio hivyo ili wakawe mabalozi wazuri wanapokuwa nchini kwao.


Aliwataka wanapata tena fursa warudi nchini kuitembelea zaidi Zanzibar pia waitangaze sana wanapokuwa Afrika ya Kusini na maifa mengine kwa ujumla kupitia utalii wa michezo.


Rais Dk. Mwinyi alisema, Zanzibar imekua na ndoto kubwa ya kufanya utalii wa michezo, hivyo ujio wa Kaizer Chief umeakisi dhana halisi ya sekta ya Utalii nchini.


Vile vile Rais Dk. Mwinyi aliwaeleza Kaizer Chief iliyoambatana na ujumbe wa watu 58 wakiwemo wachezaji na viongozi wa timu hiyo, kwamba Zanzibar ina maeneo mazuri ya kupumzikia hivyo, aliwaeleza kuitumia Zanzibar kwajili ya mapumziko yao na familia zao pia kuitangaza kimataifa kwa kutaja mazuri ya utalii waliyoyashuhudia.


Naye, Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Tabia Mauli Mwita aliushukuru uongozi wa timu ya Yanga kwa juhudi zao za kuikaribisha nchini, timu ya Kaizer Chief sambamba na kumueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba ujio wa timu ya Afrika Kusini nchini ni kuendeleza jitihada za kuutangaza utalii wa nchi.


Pia, Waziri Tabia alimuarifu Dk. Mwinyi mwamba, ameikabidhi bendera ya taifa timu ya wanawake ya Zanzibar, chini ya umri wa miaka 18 kwenda Tanzania Bara kuiwakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya Cecafa yanayofanyika Tanzania Bara wakizishirikisha nchi mbalimbali kutoka Afrika, ikiwemo Tanzania, Burundi, Rwanda na Ethiopia.


Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais wa timu ya Yanga, Injinia Hersi Ally Said alisifu juhudi zinazofanywa na Rais Dk. Mwinyi kuitangaza nchi kiutalii kimataifa, pamoja na kukuza utalii.


Alisema, hatua ya kuifikisha timu ya Kaizer, Zanzibar ni kuungamkono juhudi zake na kuitangaza Zanzibar kimataifa na kuongeza taarifa za uwepo wa timu hiyo kisiwani Unguja hazitosambaa Afrika Kusini pekee bali na mataifa mengine ya dunia.


“Hatua ya kuileta Zanzibar, Timu ya Kaizer Chiefs, yenye historia barani Afrika ni sababu ya kuitangaza Zanzibar kimataifa na kufungua milango kwa wageni wengine kuja kutembelea vivutio vya utalii vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla” alieleza Hersi.


Alisema anaimani kubwa na Kaizer Chiefs, kwamba ikiondoka nchini itakua imeitangaza zaidi Zanzibar Kimataifa kupitia mashabiki wao wa Afrika ya Kusini na mataifa mengine ya dunia.


Pia, Injinia Hersi alimueleza Rais Mwinyi kwamba timu ya Yanga imekua ikishiriki mashindano ya muhimu ya Mapinduzi Cup yanayofanyika Zanzibar na kuahidi kwamba timu hiyo imejipanga kwa kikosi maalumu kushiriki tena mashindano yajayo.


Alieleza, ujio wa mabingwa hao kutoka Afrika kusini “Kaizer Chief” ni heshima kubwa nchini pia kuitembelea Zanzibar, alisema ugeni huo ulikwenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya wananchi ilivyofanikisha kuwapokea wageni kufuatia mwaliko waliowatumia na kuongeza kuwa wiki ya wananchi kwa timu yao ya Yanga iliyoanza Julai 15 na kuhitimishwa Julai 22 mwaka huu. 


Timu ya Afrika Kusini Kaizer Chief ilifanikiwa kutembelea maeneo machache ya Zanzibar kujiondea utajiri na uzuri wa haiba ya Kisiwa cha Unguja.

IMETOLEWA NA 

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI