Header Ads Widget

PPRA YALIA NA RUSHWA KWA WATENDAJI NA MAAFISA WA SERIKALI

 


Na Hamida Ramadhan Dodoma Matukio Daima APP Dodoma


MAMLAKA ya Udhibiti Ununuzi wa Umma PPRA imekuwa ikikabiliwa na hatari kubwa ya  rushwa kwa Watendaji na maafisa serikalini kwa kutoa mikataba au kuwapa faida zisizo halali wazabuni wasio na sifa.


Afisa Mtendaji Mkuu kutoka PPRA Eliakim Maswi ameyasema hayo leo jijini hapa wakati akieleza mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2023/2024


 Ameeleza , kumekuwepo na vitendo vya rushwa katika mchakato wa Ununuzi wa Umma hali inayopunguza ushindani na kusababisha upotevu wa fedha za Umma.


" Wanao hisiwa na kulalamikiwa  kuwa wanajihusisha  na vitendo hivyo viovu vya rushwa ni pamoja na Watendaji na maafisa waliomo serikalini," Amesema Afisa Mtendaji Mkuu huyo Maswi.


Aidha Amesema ,Suala la uwazi usiyoridhisha kwenye mchakato wa zabuni imekuwa ukisababishwa Changamoto za upatikani wa taarifa za zabuni, thamani ya mikataba na kuelekea ukosefu wa uaminifu na Imani.


" Ukosefu wa uwazi katika mchakato wa Ununuzi wa Umma kunasababisha Changamoto za upatikanaji wa taarifa Hali inayopelekea kukosekana kwa Imani kwa taasisi za Umma pia wananchi kukosa Imani na serikali Kutokana na Matumizi yasiyoeleweka," Amesema Mtendaji Maswi.


Ameeleza  Changamoto nyingine ni pamoja. Na mchakato wa zabuni kuchukua muda mrefu ambapo Amesema ,Ni takwa  la kisheria kufuata taratibu na kanuni za Ununuzi wa Umma ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za ushindani na taratibu zingine zinazohusiana nazo.


" Hatua hizi za kisheria Mara nyingi huongeza muda wa mchakato wa Ununuzi Hata hivyo watumishi wasio waadilifu wanakuwa ndio sababu ya Zabuni kuchukua muda mrefu," Amesema


MWELEKEO WA SERIKALI KATIKA UNUNUZI WA UMMA

 

Amesema Serikali imeendelea kidhibiti Matumizi ya Fedha za Umma kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mifumo ya kielektroniki ili kuleta tija na ufanisi unaostahili katika utekelezaji wa bajeti husika.


Amesema kwa mujibu wa sheria ya Ununuzi wa Umma ,Mamlaka imekasimiwa jukumu la kusanifu ,kuanzisha nakuhusisha mifumo mbalimbali ya kielektroniki kwa ajili ya kuweka uwazi na kuleta tija kwenye Ununuzi wa Umma.


"Kwa kuzingatia Changamoto zilizopo , Serikali ikifanya manunuzi ya kujenga Mfumo mpya unaojulikana kwa jina la " National e-procurement System of Tanzania (NeST) Mfumo unaopatikana kwa kupitia anuani ya  https://www.nest.go.tz," Amesema Mtendaji hiyo.


Na kuongeza" Ifikapo Tarehe 1 Oktoba 2023 ,taasisi nunuzi zote za serikali hazitoweza kutumia mialiko ya Zabuni kwenye Mfumo wa TANePS na badala yake zitapaswa kutumia Mfumo wa NeST," Amesema Afisa Mtendaji Maswi.

Hata hivyo Amesema baada ya Tarehe hiyo Mfumo wa TAN ePS hautopatikana hewani kwa ajili ya Matumizi ya Ununuzi wa Umma isipokuwa kwa shughuli za ndani Kama kupata taarifa za Ununuzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI