Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Ili kuanza vyema kwa maandalizi ya ligi ya mkoa wa Njombe mbunge wa viti maalum mkoa ambaye ni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Balozi Dokta Pindi Chana ametoa shilingi milioni 5 katika chama cha mpira mkoa tayari kwa ligi hiyo.
Akikabidhi fedha hizo Mbunge Chana amesema kwa kuwa yeye amekuwa mdau mkubwa wa michezo nchini na ni mbunge wa mkoa wa Njombe aliamua kutoa fedha yake mfukoni ili kuunga mkono michezo ndani ya mkoa wake huku akisema mwezi Agosti mkoa wa Njombe utakuwa mwenyeji wa Tamasha kubwa la michezo la kitaifa.
Aidha Waziri Chana ameeleza kuwapo kwa mpango wa kuanza ukarabati wa viwanja vya michezo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema miongoni mwa wadau wakubwa wa michezo katika mkoa wa Njombe ni Mbunge Pindi Chana na hivyo waliona ni muhimu wamshirikishe katika kuunga mkono jitihada za michezo katika mkoa.
Mwenyekiti wa kamati ya michezo mkoa wa Njombe Judica Omary ambaye ni katibu Tawala mkoa Amesema wanaendelea kutekeleza maelekezo yote ya serikali ya kuhakikisha miundombinu ya michezo ikiwemo kutenga viwanja vya michezo kwenye kila shule inatekelezwa.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mpira mkoa wa Njombe NJOREFA Mwalimu Mstaafu Meshack Mnyawasa amekiri kupokea fedha hizo na kuwaagiza viongozi wake kwenda kuzifanyia kazi iliyokusudiwa.
Pia Mnyawasa, amemuomba waziri kupeleka maombi shirikisho la mpira Tanzania (TFF) kupata kituo cha mabingwa wa mikoa ili kuweza kupandisha timu ligi kuu
0 Comments