Header Ads Widget

UPINZANI HAUJAWAHI KUSHINDA ZANZIBAR - KHAMIS MBETO

 




Na THABIT MADAI, Zanzibar -MATUKIO DAIMA APP



Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema madai ya  Balozi Ali Karume kuhusu  uchaguzi mkuu akisema CCM haikushinda  si mageni kwani  aliyekuwa Makamo Mwenyekiti  CUF Mussa Haji Kombo amewahi kutamka mgombea urais  wa CUF  hayati Maalim Seif Sharif Hamad hakuwahi kushinda urais .



Hadi leo hakuna ushahidi wowote unaoonyesha upinzani umeshinda  kama Act wazalendo kinavyotaka kueneza madai hayo.



Ufafanuzi huo umetolewa na katibu wa kamati maalum  ya Nec zanzibar , Mbetto  Khamis Mbetto , akijibu tuhuma za katibu wa Habari,Uenezi  na Mawasiliano kwa umma , Salum  Bimani alipohutubia mkutano wa hadhara huko.....



Mbetto alisema madai ya baadhi ya wanasiasa ambao matlaba yao kisiasa hayakufikiwa na  kutamka majukwaani kuhusu  uchaguzi ,wana hamaki na jazba ili kuvuruga upepo pale wanaposhindwa au wakipovuliwa  uanachama.



Alisema Kombo na  Karume  hawajawahi kuwa wenyeviti au maafisa wa Tume  ya uchaguzi Zanzibar (zec)  hivyo hawana haki kimamlka na kisheria kusikilizwa au kuzungumzia  matokeo  ya uchaguzi  wakati wowote.



"Madai  ati CCM  haijashinda wakati  inaongoza serikali ni upuuzi unaostahiki kupuuzwa. Hata Kombo  amewahi kusema  Maalim Seif hakushinda uchaguzi wowote zanzibar  .Maalim seif na kina  Bimani  hawajakanusha madai hayo mpaka leo  "Alisema Mbetto.



Aidha katibu huyo Mwenezi ccm zanzibar alisema kinachoonekana kwa  viongozi wa Act wazalendo  wanataka kuibeba kauli ya Balozi Mstaafu  Karume wakidhani utakuwa ndio  mtaji  mpya kisiasa utakaowapa manufaa .



"CCM iweje kisishinde wakati ndicho kinachominiwa na wananchi. Wazanzibari si wajinga hadi wauchague upinzani kwa kubahatisha . CCM kimeshinda chaguzi zote na kitaendelea kushika madaraka na kuiongoza  zanzibar"  Alisisistiza 



Katibu huyo Mwenezi alidai kombo aliwahi kusema CUF kulikuwa na uhodari  wa kueneza propaganda  hasi kwa nguvu hasi zikalubalika kitaifa na kimataifa na kulikuza jambo lolote lakini hakuna ushahidi  CUF au ACT Wazalendo vilishinda.



"CUF walitaka wawe na makamishna wao ndani ya Zec pia hawashinda.Wakataka Daftari la kudumu la  wapiga kura hawakupata ushindi . Wakaomba kuwe na kadi za  mzanzibar mkaazi  hawakupata ushindi. Ni chama kisicho na sera za matumaini hivyo ni vigumu kushinda" alieleza



Akizungumzia maendeoeo yanayokuza lwa kasi chini yabuongozi wa raia wa zanzibar Dkt Hissein Ali Mwinyi,Mbetto alisema ni jambo linaloupa hofu upinzani kwani wanajua mwaka 2025 hawatakuwa na hoja dhidi ya uatawala wa  CCM awamu ya nane.



Hata hivyo alimtaka Rais Dkt Mwinyi kuendelea na utekelezaji wa ilani ya ccm  hatua lwa hatua na kusema kuwa siku zote madebe matupu lamwe hayataacha kupiga kelele .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS