Header Ads Widget

TUNAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA SIKOSELI NCHINI - DKT. SHEKALAGHE




Na. WAF - Dodoma


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe mapema leo amekutana na timu ya wawakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) wanaosimamia mradi wa Sikoseli nchini wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Appolinary Kamuhabwa.


Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara Jijini Dodoma Katibu Mkuu Dkt. Shekalaghe ameihakikishia timu hiyo juu ya kuendelea kuboresha Sekta ya Afya hususan katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa Sikoseli nchini.


“Juhudi zinaendelea kufanywa na Serikali na wadau mbalimbali katika huduma za kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa Sikoseli zikiwemo tafiti za kisayansi, upatikanaji wa matibabu ya hali ya juu kwa wagonjwa wa Sikoseli kama ubadilishaji damu na upandikizaji uloto.” Amesema Dkt. Shekalaghe



Aidha, wamejadiliana ukubwa wa ugonjwa wa Sikoseli nchini ambapo Mkurugenzi wa Jumuia hiyo Bi. Arafa amesema kuwa, watoto 11,000 hadi 14,000 huzaliwa na ugonjwa wa Sikoseli kila mwaka na inakadiriwa kuna jumla ya wagonjwa ni 200,000 wa Sikoseli nchini Tanzania. 


Vile vile, timu hiyo imesema kuwa takribani asilimia 12 hadi 20 ya Watanzania wana vinasaba vya Sikoseli ambao wanaweza kupata watoto wenye ugonjwa wa Sikoseli na kuongeza idadi ya wagonjwa wenye ugonjwa huo hapa nchini.



Timu hiyo iliyoongozwa na Prof. kamuhabwa ameambatana na Makamu Mkuu wa Chuo Elimu na Matafiti Mkuu wa Mradi wa Sikoseli Prof. Emmanuel Balandya, Mkurugenzi wa Jumuiya ya wagonjwa wa Sikoseli Tanzania Bi. Arafa Saidi, Watafiti katika mradi wa Sikoseli Dkt. Irene Minja, Dkt. Siana Nkya na Lulu Chirande

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS