Header Ads Widget

MAJI YA BOMBA YAENDELEA KUSAMBAZWA MUSOMA VIJIJINI

 


NA MWANDISHI WETU, MUSOMA VIJIJINI.


VIJIJI vya Bwasi, Buganda na Kome vinatarajiwa kupata maji hivi karibuni kufuatia Kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya Maji ya RUWASA ya kutekeleza miradi ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye vijiji hivyo ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.


Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Mbunge Jimbo Musoma Vijijini, imebainisha kuwa tenki la ujazo la lita 150,000 linajengwa katika Kijiji cha Bwasi huku likitarajiwa kukamilika Juni 30, mwaka huu.


"Shukrani za dhati zinatolewa kwa Serikali yetu inayoongozwa na Mhe Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusambaza maji safi na salama ya bomba vijijini mwetu.


Upanuzi huu unafanyika ili maji ya bomba la Bujaga-Bulinga-Busungu yasambazwe na kutumiwa kwenye Kata ya Bwasi yenye Vijiji vitatu (Bugunda,Kome na Bwasi)." Imebainisha taarifa hiyo na kuongeza kuwa:


"Gharama ya mradi ni Tsh 997,714,196.Urefu wa mtandao wa usambazaji maji KM 31.5 na vitekea maji 35." Imebainisha taarifa hiyo.


Aidha, Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21, lina Vijiji 68 vyenye Vitongoji 374 ambapo Vijiji vyote vina miradi ya maji ambayo iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji." Imebainisha taarifa hiyo.


Pia taarifa hiyo Imebainisha kuwa, Bomba la Bujaga-Bulinga-Busungu

Maji ya bomba hilo yanatoka Ziwa Victoria na mashine imejengwa Kijijini Bujaga (Kata ya Bulinga)


"Tenki la ujazo wa lita 200,000 limejengwa Kijijini Busungu na lingine la lita150,000 limejengwa Kijijini Bulinga.


Maji kutoka kwenye matenki hayo ndiyo yanasambazwa  kwenye Vijiji vya Bukima (Kata ya Bukima) na Kwikerege (Kata ya Rusoli).




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI