Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
JAJI Mkuu, Profesa. Ibrahim Hamis Juma ameitaka mahakama kuhakikisha safari ya kuhamia Dodoma inafanyikia kidigitali mabadala ya Kuhama kianalogi kwa maroli ya mabox ya makaratasi.
Jaji mkuu ametoa kauli hiyo jijini Dodoma, wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania.
Amesema safari ya kuhamia Dodoma ni lazima ifanyike na si kianalogia na wasipokuwa na elimu ya kidigital watahama kianalogia na kuwataka kulikataa hilo mapema .
Amesema Watumiaji wa Mahakama na wananchi watategemea kila mtumishi wa Mahakama aonyeshe na kudhihirisha kuwa Maboresho hayaishii katika kukamilisha majengo ya kisasa yaliyounganishwa na mifumo ya kisasa ya teknolojia.
"Wananchi na watumiaji huduma za Mahakama wanataka utamaduni mpya wa utoaji haki uliotokana na hayo maboresho ya mahakama. Ubora wa Majengo unapimwa kwa ubora wa huduma inayopatikana kutoka katika majengo,"amesema.
UMUHIMU WA TEHAMA KATIKA UJENZI WA UTAMADUNI WETU WA KIMABORESHO
Ametumia Baraza hilo kuendelea kuwakumbusha kuwa utoaji wa huduma kwa umma katika Karne ya 21 ni tofauti kabisa na ilivyokuwa miaka michache tu iliyopita. Hivi karibuni, tumeona juhudi kubwa za Serikali ya Tanzania kuongeza matumizi ya TEHAMA katika karibu kila nyanja ya utoaji wa huduma za umma.
"Naomba nitumie Baraza hili kutambua mchango mkubwa katika kuleta ufanisi uliotokana na matumizi ya TEHAMA,"amesema Jaji Mkuu.
Amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatekeleza Mpango wa Dijitali Tanzania (Digital Tanzania Project).
Pia ametaja malengo ya Mradi huo kuwa ni kuongeza upatikanaji wa huduma za umma kwa urahisi, ubora, uwazi, ufanisi na kwa bei nafuu.
0 Comments