Jeshi la Polisi Tanzania jioni ya leo limethibitisha kuwa Makachero wa Tanzania wamewakamata Raia watatu wa Afrika Kusini ambao ni Thabo Bester maarufu kwa jina la ‘Mbakaji wa Facebook’, Mpenzi wake Dr. Nandipa Magumana na Zakaria Alberto.
Inadaiwa watatu hao wamekamatiwa Arusha japo taarifa rasmi ya Polisi haijasema eneo walikokamatiwa, kwa upande mwingine Msemaji wa Polisi Makao Makuu David Misime amesema taratibu za mawasiliano ya kisheria ya ndani na ya kimataifa zinaendelea kukamilishwa.
Itakumbukwa kuwa Thabo amekuwa akisakwa na Polisi wa Afrika Kusini akikabiliwa na kosa la kughushi kuwa amefariki alipokuwa gerezani na kutoroka kisha baadaye ikabainika kuwa hajafariki, kitendo ambacho kiliishangaza Nchi nzima.






0 Comments