Askofu mstaafu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa, Profesa Owdenburg Mdegela, amekemea matendo ya ushoga au mahusiano ya jinsia moja ambayo yanaonekana kukua kwa kasi ulimwenguni, na kusema hali hiyo imekuwa mbaya hadi kufikia hatua kwa baadhi ya makanisa kujingiza wazi wazi katika ushoga.
Askofu, Profesa Mdegela ameyasema hayo leo April 7, 2023 katika ibada ya Ijumaa kuu, iliyofanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa kanisa kuu Iringa na kuongeza kuwa wakristo wanapoazimisha siku ya Ijumaa Kuu ya kuteswa kwa Yesu Kristo, wanatakiwa kutafakari matendo yao upya.
Pia ameongeza kuwa kwa sasa kanisa linaharibiwa na makundi ya wanasayansi, wanasiasa, wathiolojia na mitume na manabii wa uongo ambao wengi wao hawataki mahubiri ya ukweli na badala yake wabakia kupotosha jamii kwa malengo yao binanfsi.
“Hivi sasa wameibuka watumishi wanaojiita maanabii na mitume lakini kazi yao kubwa ni kupotosha jamii kutokana kutokuwa na elimu ya Thiolojia na wengine wakiambiwa wakasome wanakataa kwa madai ya kufunuliwa na Mungu”
Pia amewataka wakristo kuachana na tabia ya kumwamini mwanadamu kwa kisingizio cha utumishi wa Mungu kwani kwakufanya hivyo kuonyesha jinsi gani wameshindwa kulifahamu neno la Mungu pamoja na kukosa maarifa ambayo yanasababisha waumini wengi kudanganywa na watumishi wa uongo.























0 Comments