Header Ads Widget

WAZIRI MWIGULU AWASILISHA MAPENDEKEZO YA SERIKALI YA MPANGO WA TAIFA WA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24



Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amewasilisha mbele ya Bunge Jijini Dodoma, Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, ambapo amesema Serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 44,388.1 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo.



 Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 29,232.1 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikijumuisha shilingi bilioni 12,771.5 kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali na gharama nyingine za Mfuko Mkuu na shilingi bilioni 10,882.1 kwa ajili ya mishahara ikiwemo upandishaji wa madaraja kwa watumishi na ajira mpya, na shilingi bilioni 6,396.9 kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC).


Matumizi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa shilingi bilioni 15,156.0. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 11,873.9 ni fedha za ndani, sawa na asilimia 78.3 ya bajeti ya maendeleo na shilingi bilioni 3,282.1 ni fedha za nje. Ukomo wa fedha za maendeleo upo ndani ya wigo wa kati ya asilimia 30 na 40 ulioanishwa kwenye Mpango Elekezi wa Muda Mrefu (2011/12 – 2025/26). 


Utengaji wa fedha za maendeleo umezingatia miradi inayoendelea ikiwemo miradi ya kimkakati na ya kielelezo pamoja na utekelezaji wa miradi kupitia utaratibu wa PPP ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kugharamia miradi ya maendeleo kwa utaratibu uliozoeleka.



 Aidha, bajeti ya matumizi ya kawaida imeongezeka kufuatia kukamilika kwa miradi ya maendeleo hususan kwenye sekta za huduma za jamii ambazo kwa sasa zinahitaji fedha za matumizi ya kawaida kwa ajili ya uendeshaji.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI