Walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari Wilayani Malinyi wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa sensa Elimu ya msingi (ASC)na mfumo wa taarifa za shule (SIS)kwa shule za msingi na sekondari.
Mafunzo hayo ya siku nne yamewahusisha walimu wakuu wote wa shule za sekondari na msingi wilayani humo yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo walimu kuufahamu mfumo huo wa kina.
Mbali na walimu wakuu wa shule za sekondari na msingi pia maafisa elimu kata ,maafisa elimu watu wazima,elimu maalum na maafisa ustawi wa jamii pia wamepatiwa mafunzo hayo.
Mafunzo kwa walimu na maafisa hao imetolewa kwa awamu mbili ambapo awali yalifanyika katika tarafa ya Mtimbira Machi 24 na 25 huku tarafa ya Malinyi na Ngoheranga yakifanyika Machi 26 na 27.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisi ya wakuu wa Divisheni za elimu msingi na sekondari halmashauri ya wilaya ya Malinyi ni kuwajengea uwezo walimu wakuu na maafisa hao kuhakikisha takwimu zinzokusanywa katika ngazi za shule na vituo vya kulelea Watoto wadogomchana zinakuwa sahihi,halisi na zinazingatia muda na zenye mwendelezo na kuhusiana.
0 Comments