Header Ads Widget

NMB YATOA MILIONI 120 MAANDALIZI YA UZINDUZI MWENGE KITAIFA





Zaidi ya shilingi milioni 120 zimetolewa na Benki ya NMB kwaajili ya maandalizi uzinduzi wa mwenge kitaifa unaofanyikia Mkoani Mtwara mbali na pesa pia wametoa vifaa mbalimbali kwaajili ya watoto wa halaiki.


Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Kaimu Meneja wa Kanda ya Kusini Nmb Roman Degereki alisema kuwa wametoa zaidi ya shilling mil 120 za kitanzania kwaajili ya kukamilisha maandalizi ya uzinduzi wa mwenge kitaifa.


“Tumetoa miamvuli 1000, tracksuit 1000 pamoja na tshirt 300 za wadau mbalimbali watavaa katika uzinduzi wa mwenge kitaifa ikiwa ni sehemu ya huduma ambazo tumetoa nchini kwa kwa zaidi ya miaka 25 na tunaendelea kutoa huduma hiyo” alisema Degeleki



“Tumetoa vifaa hivyo ili kuwezesha zeozi hili kukamilika kwa wakati ili kuisaidia serikali katika kukamilisha na kupendezesha zoezi hilo” alisema Degeleki 


kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas alisema kuwa kwa kiasi kikubwa tunaishukuru benki ya NMB  kwakutushika mkono.



“Tunashukuru jitihada za NMB katika mkoa wetu tulipokuwa na jambo hili la uzinduzi wa mwenge tuliwaomba kama wadau ili waweze kufanikisha jambo hilo ambapo wametuunga mkono kwakutupatia tracksuit 1000, miavuli 1000 pamoja na tshirt 300”


“Tumezipokea kwaajili ya tukio hili la uzinduzi wa mwenge pamoja na michango mingine mbalimbali na pesa zaidi ya shilingi milioni 25 wamekuwa wazalendo wakubwa zaidi nafarijika kupokea vifaa hivi ili viweze kufanyiwa majaribio na kuweza kugawiwa kwa vijana”




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI