Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Katika mtaa wa Mpechi mjini Njombe kumeripotiwa kutokea kwa tukio la ubakaji uliofanywa na anayedaiwa kuwa ni baba wa kufikia wa mtoto mwenye umri wa miaka 8 ambaye jina lake limehifadhiwa.
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe linamshikilia mtuhumiwa huyo Bwana Menrad Mbigi mwenye umriwa mika 28 mkazi wa mtaa wa mpechi mjini njombe kwa tuhuma za kubaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka 8 tukio ambalo linahusishwa na imani za kishirikina.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema mtuhumiwa wamemkamata machi 13 mwaka huu ambapo mtoto wa mke anayeishi naye alikuwa akimfanyia vitendo hivyo huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.
Kamanda Issah Amesema jeshi la polisi litahakikisha linamtafuta na kumkamata hadi mtu aliyemshawishi mtuhumiwa huyo kufanya tukio hilo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mpechi mjini Njombe Onesmo Kilasi amesema awali alipata taarifa za kuwapo kwa mtu anayejihusisha kimapenzi na mtoto huyo kisha akaanza ufuatiliaji hadi alipobaini ukweli huo kwani balozi wa eneo hilo alipoongea na mke wa mtuhumiwa huyo alikiri kuwa mumewe alianza kutekeleza vitendo hivyo kwa muda mrefu.
Badhi ya wananchi mjini Njombe akiwemo Alex Msigwa na Oresta Mwalongo wameonesha masikitiko yao juu ya ukatili unaondelea katika jamii kwani vinapaswa kupigwa vita na kila mtu huku jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola vikitakiwa kuchukua hatua kali za kisheria.
0 Comments